1Msingi wa Kanisa Ndiye Yesu Bwana;Kiumbe chake kipya Akipenda sana; Kutaka ‘kitafuta Alishuka chini, Naye kwa haja yake, Akafa Mtini.2Lina kila kabila Kisha ndiyo moja Wokovu wake una Mwokozi ndiyo moja; Uzazi ni umoja. Moja tumaini. Chakula ni kimoja. Moja tumaini.3Watu hustaajabu Kwa mashaka yote. Yaipatayo nje Hata ndani mwote; Ila watakatifu Humwomba, wakikesha Usiku ni kilio. Asubuhi raha.4Mashaka na taabu Hata vita vyake. Vyangoja matimizo Ya amani yake. Ndipo kwa macho yetu Twone utukufu Kanisa ya kushinda itastarehe juu.