Advent Hymnals
172. MFALME AJAPO
Nyimbo Za Kristo,
1
Mfalme wetu atuita tukae karamuni kwake;
Itakuwaje nasi kule Bwana ajapo?
Chorus
Bwana ajapo, ndugu, Bwana ajapo!
Itakuwaje na sisi, Bwana akija?
2
Atavikwa vizuri sana, taji badala ya miiba;
Kweli tokeo la fahari Bwana ajapo.
3
Kwa furaha awakubali wenye mavazi ya arusi;
Tu wa heri tukimridhisha Bwana ajapo.
4
Kutakuwako na utengo: watalia waliomwasi;
Cha kutisha kitambo kile Kristo ajapo!
5
Mfalme utupe neema sisi tunapokungoja,
Tusiogope kukuona ujapo Bwana.
- Title Mfalme Ajapo Key Titles undefined First Line Mfalme wetu atuita tukae karamuni kwake; Author Year Composer Hymnal - Tune Metrical pattern # Stanzas Chorus Chorus Type Subjects Texts Print Texts Scripture Song