Advent Hymnals

177. KAZI YANGU IKIISHA

Nyimbo Za Kristo,


1
Kazi yangu ikisha,nami nikiokoka;
Na kuvaa kutokuharibika,
Nitamjua mwokozi nifikapo ng`amboni;
Atakuwa wa kwanza kunilaki.

Chorus
Nitamjua,Nitamjua,nikimwona uso kwa uso;
Nitamjua,Nitamjua,kwa alama za misumari.

2
Furaha nitapata nikiona makao`
Bwana aliyotuandalia;
Nitamsifu Mwokozi kwa rehama na pendo;
Vilivyonipa pahali mbinguni.

3
Nao waliokufa katika Bwana Yesu,
Nitawaona tena huko juu;
Lakini nifikapo kwake huko mbinguni,
Nataka kumwona Mwokozi kwanza.

4
Milangoni mwa mji Bwana atanipisha,
Pasipo machozi wala huzuni.
Nitauimba wimbo wa milele;lakini
Nataka kumwona mwokozi kwanza.




  • -
    Title Kazi Yangu Ikiisha
    Key
    Titles undefined
    First Line Kazi yangu ikisha,nami nikiokoka;
    Author
    Year
    Composer
    Hymnal -
    Tune
    Metrical pattern
    # Stanzas
    Chorus
    Chorus Type
    Subjects
    Texts
    Print Texts
    Scripture Song