Advent Hymnals

176. ATI TUONANE MTONI

Nyimbo Za Kristo,


1
Ati tuonane mtoni? Maji mazuri ya mbingu; 
Yanatokea mwangani, penye kiti cha Mungu.

Chorus
Naam, tuonane mtoni! Watakatifu, kwenu ni mtoni! 
Tutakutanika kule mtoni penye kiti cha Mungu.

2
Tukitembea mtoni na Yesu Mchunga wetu,
Daima tu ibadani usoni pake kwetu.

3
Tukisafiri mtoni tutue ulemeao
Wema wa Mungu yakini; una taji na yao!

4
Kwang`ara sana mtoni cha Mwokozi ni kioo, 
Milele hatuachani tumsifu kwa nyimbo.

5
Karibu sana mtoni, karibu tutawasili, 
Mara huwa furahani na amani ya kweli.  



  • -
    Title Ati Tuonane Mtoni
    Key
    Titles undefined
    First Line Ati tuonane mtoni? Maji mazuri ya mbingu;
    Author
    Year
    Composer
    Hymnal -
    Tune
    Metrical pattern
    # Stanzas
    Chorus
    Chorus Type
    Subjects
    Texts
    Print Texts
    Scripture Song