1Hapo Yesu atakapoita mataifa mbele yake, Tutashindaje kwenye hukumu mbele ya kiti cha enzi? ChorusAtakusanya ngano ghalani, atatupambali makapo; Tutashindaje hukumuni siku kuu ya kiyama? 2Je, tutasikua neno tamu: "vema, wewe mtumwa mwema," Ama wenye uchunguna hofu tutakatazwa ufalme? 3Atakubali tu kwa furaha watoto wake wapendwa, Atawapa mavazi meupe, wakea tayari kumlaki. 4Hivyo tukeshe, nasi tungoje, wenye taa zinazo waka; Tutakapoitwa arusini tuwe tayari kumlaki. 5Roho ikielekea mbingu twangoja wenye saburi, Hata safari yetu iishe, tukae kwake milele.