Advent Hymnals
164. MISHALE YA NURU
Nyimbo Za Kristo,
1
Unakaribia wakati wa Kuja kwa Yesu.
Atawachukua watu wake Nyumbani juu.
Chorus
Tunaiona mishale ya nuru Inayopenya giza;
Tunaiona mishale ya nuru Ya ufunuo.
2
Injili inatangazwa pote kwa mataifa;
Bwana wa Arusi atakuja Na tarumbeta.
3
Pamoja na malaika zake Bwana arudi,
Awapeleke waaminifu Wasife tena.
4
Wapenzi waliotengwa kale Watakutana;
Machozi yao wenye huzuni Yatafutika.
- Title Mishale Ya Nuru Key Titles undefined First Line Unakaribia wakati wa Kuja kwa Yesu. Author Year Composer Hymnal - Tune Metrical pattern # Stanzas Chorus Chorus Type Subjects Texts Print Texts Scripture Song