Advent Hymnals
170. JINA LANGU LIMEANDIKWA JE
Nyimbo Za Kristo,
1
Sitafuti mali, wala utajiri; Nataka kwa yakini nipate Mwokozi.
Chuoni mwa Ufalme, niambie Yesu, Jina langu yakini limeandikwa, je?
Chorus
Limeandikwa, je? Jina langu huko?
Kitabuni mbinguni, limeandikwa, je?
2
Dhambi zangu ni nyingi, ni kama mchanga, Lakini damu yako, Mwokozi, yatosha;
Kwani umeahidi: zijapo nyekundu Zitakuwa nyeupe ilivyo theluji.
3
Mji mzuri sana, wa majumba makuu, Walipo malaika, mji bila ovu;
Wakaapo walio na mavazi safi, Limeandikwa sasa, jina langu huko?
- Title Jina Langu Limeandikwa Je Key Titles undefined First Line Sitafuti mali, wala utajiri; Nataka kwa yakini nipate Mwokozi. Author Year Composer Hymnal - Tune Metrical pattern # Stanzas Chorus Chorus Type Subjects Texts Print Texts Scripture Song