1Pengine ni saa ya kupambazuka,Mishale ya jua ipenyapo giza,Kwamba atakuja Yesu mtukufu,Awapokee wake. Bwana itakuwa lini Tutapoimba,"Anakuja, Bwana Yesu, Aleluya,Amin, Aleluya, Amin?"2Pengine mchana, pengine jioni,Pengine usiku wa manane, giza,Itatoweka kwa fahari akija,Awapokee wake. 3Majeshi yake yataimba "Hosana,"Na watakatifu waliotukuzwa,Watamsifu kwa kuwa amekuja,Awapokee wake. 4Furaha tukiitwa pasipo kufa,Pasipo kuona maradhi, machozi;Kuchukuliwa winguni kwa fahari,Akija kwa watu wake.