Advent Hymnals
154. YANIPASA KUWA NAYE
Nyimbo Za Kristo,
1
Yanipasa kuwa naye, Mwokozi Bwana wangu.
Akiwa karibu nami, napata nguvu kweli.
Chorus
Moyo hauogopi, wala kutikisika.
Nitakwenda apendapo, kwa kuwa anilinda.
2
Yanipasa kuwa naye, kwani nategemea;
Anaweza kufariji na maneno matamu.
3
Yanipasa kuwa naye maisha yangu yote;
Yakiwapo majaribu na mashaka yo yote.
4
Yanipasa kuwa naye katika njia zangu;
Macho yake yaongoza hatua zangu zote.
- Title Yanipasa Kuwa Naye Key Titles undefined First Line Yanipasa kuwa naye, Mwokozi Bwana wangu. Author Year Composer Hymnal - Tune Metrical pattern # Stanzas Chorus Chorus Type Subjects Texts Print Texts Scripture Song