1U mwendo gain nyumbani? Mlinzi akanijibu, "Usiku sasa waisha, macheo karibu."Usihuzunike tena, bali ulemee mwendo Hata ushike ufalme kule mwangani juu. 2Na tena niliuliza, nchi yote ikajibu; "Sasa mwendo watimika, milele karibu." Usihuzunike tena, ishara kuu zasonga Na viumbe vyangojea sauti ya Bwana.3Nikamwuliza shujaa, ndivyo kanitia moyo:"Shikilia mapigano, kitambo yaisha." Usihuzunike tena, kazi ifanywe kwa moyo; Tumeahidiwa tunu tuishapo shinda.4Siyo mbali na nyumbani! Fikira tamu njiani,Latupoza roho, nalo lafuta machozi.Usihuzunike tena, kitambo tutakutana Wenye furaha kamili nyumbani mwa Baba