1Anakuja upesi, Yesu Bwana wetu,Msafiri mbali na kwao;Alisema dhahiri, "Nitakuja tena"; Amina; na uje, E Bwana. ChorusYuaja, Yesu atarudi sasa;Anakuja duniani.Wasafiri wote watapumzika,Yesu anaporudi tena.2Makaburi yote wafu wanapolala,Yatafunguliwa tena;Na mamilioni pale wataondoka tena,Wasione machozi kamwe.3Hatutatengana na hao tena huko;Nyimbo nzuri tutaimba.Watakusanyika `toka kila kabila,Miguuni pa Mwana-Kondoo.4Aleluya Amin! Aleluya tena!Upendo wake unashinda!Tutamsifu milele, hata tutashangaa,Jinsi alivyotukomboa.