Advent Hymnals

147. UISHI NDANI YANGU

Nyimbo Za Kristo,


1
Tawala ndani yangu, Ee Yesu, Mfalme. 
Uwe kwangu majibu Kwa maswala yangu;
Uishi ndani yangu, Wewe, mwongozi
Utumishi ni wangu, Wako utukufu.

2
Hekalu nimetoa, Umelisafisha;
Sasa fahari yako Imulike ndani;
Dunia iwe kimya, Mwili sasa uwe 
Mtumwa mtulivu Wa kukutii tu. 

3
Viungo vyake mwili, Vyote vikungoja 
Tayari vikiitwa Kwenda, kusimama; 
Bila manung`uniko Au malaumu, 
Au kusumbuliwa, Pasipo majuto.

4
Niwe na utulivu Pasipo haraka; 
Tayari kungojea Maagizo yake. 
Tawala ndani yangu. Ee Yesu, Mfalme, 
Uwe kwangu majibu Kwa maswali yote. 



  • -
    Title Uishi Ndani Yangu
    Key
    Titles undefined
    First Line Tawala ndani yangu, Ee Yesu, Mfalme.
    Author
    Year
    Composer
    Hymnal -
    Tune
    Metrical pattern
    # Stanzas
    Chorus
    Chorus Type
    Subjects
    Texts
    Print Texts
    Scripture Song