Advent Hymnals

146. TWAE WANGU UZIMA

Nyimbo Za Kristo,


1
Twae wangu uzima, Sadaka ya daima;
Twae saa na usiku, Zikutukuze huku.

2
Twae mikono nayo, Ifanye upendavyo,
Twae yangu miguu, Kwa wongozi wako tu.

3
Twae sauti yangu, Niimbe kwa Mungu tu;
Itwae na midomo, Ijae neno lako.

4
Twae dhahabu pia, Na yote ya dunia;
Twae yangu hekima, Upendavyo tumia.

5
Nia itwae, Mungu, Haitakuwa yangu;
Twae moyo; ni wako, Uwezo makazi yako.

6
Twae mapenzi yangu, Sifa za moyo wangu;
Twae kabisa nafsi, Niwe wako halisi



  • -
    Title Twae Wangu Uzima
    Key
    Titles undefined
    First Line Twae wangu uzima, Sadaka ya daima;
    Author
    Year
    Composer
    Hymnal -
    Tune
    Metrical pattern
    # Stanzas
    Chorus
    Chorus Type
    Subjects
    Texts
    Print Texts
    Scripture Song