1Chini ya msalaba Nataka simama; Ndio mwamba safarini, Wa kivuli chema;Ni kweli kwa roho yangu Ni tuo kamili, Tatua mzigo wangu Wakati wa hari. 2Hapa ni pema sana, Ni ngome kamili; Hapa yameonekana, Mapenzi ya kweli;Kama alivyoonyeshwa Yakobo zamani.Msalaba umekuwa Ngazi ya mbinguni. 3Na Yesu Msalabani Walimkemea, Alikufa niokoke Niliyepotea:Naona ajabu sana Ya mambo mawili Jinsi alivyonipenda Nisiyestahili. 4Atakayeonana Na Yesu mbinguni, Njia yake aanzapo Ni Msalabani;Wokovu upo hapa tu, Mwingine hapana. Kisha kuna furaha kuu Pamoja na Bwana.