1Saa heri ya sala tunapojidhili,Kama tukija kwake Yesu rafiki;Tukiwa na imani kwamba yu mlinzi, Waliochoka sana watapata raha.ChorusSaa ya sala, iliyo heri; Waliochoka sana watapata raha.2Saa heri ya sala, ajapo Mwokozi, Ili awasikie watoto wake.Hutwambia tuweke miguuni pake Mizigo yetu yote: tutapata raha. 3Saa heri ya sala, wawezapo kuja Kwa BwanaYesu wanaojaribiwa; Moyo wake mpole, atawarehemu; Waliochoka sana watapata raha.4Saa heri ya sala tutakapopewa,Mibaraka ya roho, tukimwamini; Kwa kuamini kweli hatutaogopa;Waliochoka sana watapata raha.