1Nitwae hivi nilivyo, umemwaga damu yako, Nawe ulivyoniita, Bwana Yesu, sasa naja.2Hivi nilivyo; langu kujiosha roho yangu; Nisamehe dhambi zangu, Bwana Yesu, sasa naja.3Hivi nilivyo; sioni kamwe furaha moyoni, Daima ni mashakani, Bwana Yesu, sasa naja.4Hivi nilivyo kipofu, maskini na mpungufu; Wewe ndiwe u tajiri, Bwana Yesu, sasa naja.5Hivi nilivyo, mimi tu, Siwezi kujiokoa; Na wewe hutanikataa, Bwana Yesu, sasa naja.6Hivi nilivyo; mapenzi yamenipa njia wazi; Hali na mali sisazi, Bwana Yesu, sasa naja.