Advent Hymnals
132. BWANA NI MCHUNGA
Nyimbo Za Kristo,
1
Bwana ni Mchunga, Sitahitaji;
Majani mabichi malisho yangu.
Ananinywesha maji matulivu;
Atanirudisha nikipotea.
2
Nipitapo bondeni mwa mauti
U mlinzi wangu sitaogopa;
Fimbo lako latosha kunilinda;
Ukinifariji sina hasara.
3
Kati ya mateso meza waandaa,
Na kikombe changu kinafurika;
Umenipaka kichwani mafuta;
Nitaulizaje zaidi kwako?
4
Wema na fadhili zinifuate
Siku zangu zote hata milele;
Nami nitakaa nyumbani mwa Bwana
Katika ufalme wa pendo lake.
- Title Bwana Ni Mchunga Key Titles undefined First Line Bwana ni Mchunga, Sitahitaji; Author Year Composer Hymnal - Tune Metrical pattern # Stanzas Chorus Chorus Type Subjects Texts Print Texts Scripture Song