Advent Hymnals

117. WAMWENDEA YESU

Nyimbo Za Kristo,


1
Wamwendea Yesu kwa kusafiwa. Kuoshwa kwa damu ya Kondoo? 
Je, neema yake yatumwagiwa? Waoshwa kwa damu ya Kondoo? 

Chorus
Kuoshwa kwa damu Itutakasayo ya Kondoo?
Ziwe safi nguo nyeupe sana; Waoshwa kwa damu ya Kondoo? 

2
Wamwandama daima Mkombozi. Waoshwa kwa damu ya Kondoo?
Yako kwa Msulubiwa  mavazi? Waoshwa kwa damu ya Kondoo? 

3
Atakapokuja Bwana-arusi Uwe safi katika damu! 
Yafae kwenda mbinguni mavazi: Yaoshwa kwa damu ya Kondoo?

4
Yatupwe yalipo na takataka; Uoshwe kwa damu ya Kondoo:
Huoni kijito chatiririka Uoshwe kwa damu ya Kondoo? 


  • -
    Title Wamwendea Yesu
    Key
    Titles undefined
    First Line Wamwendea Yesu kwa kusafiwa. Kuoshwa kwa damu ya Kondoo?
    Author
    Year
    Composer
    Hymnal -
    Tune
    Metrical pattern
    # Stanzas
    Chorus
    Chorus Type
    Subjects
    Texts
    Print Texts
    Scripture Song