1Sauti ni yake Bwana, "Kwenda nani tayari?"Mavuno yanakawia, Nani atayavuna?Kwa kudumu anaita, Zawadi atatoa;Nani atakayejibu, "Nipo Bwana nitume."2Kama huwezi safari, Hata nchi za mbali,Pana watu karibuni, Wasiomjua Yesu;Kama huwezi kusema, Jinsi ya malaika,Waweza kuutangaza, Upendo wa Mwokozi.3 Ingawa huwezi kuwa, Mkesha mlangoni,Ukiwatolea watu, Nafasi ya uzima;Kwa sala na kwa sadaka, Watoa msaada,Kama Harun mwaminifu, Kuinua mikono.4Roho za watu zikifa, Bwana akikuita,Usiseme kwa uvivu, "Hakuna kazi kwangu".Kwa furaha anza kazi, Ile aliyokupa,Ukajibu mara moja, "Nipo Bwana nitume".