Advent Hymnals
110. MLANGO WAZI
Nyimbo Za Kristo,
1
Mlango uko wa wema, Mlango wazi huo:
Yesu ameufungua Na hakuna kufunga
Chorus
Mlango wazi, ajabu, Uliachwa wazi kwangu?
Kwangu, Kwangu? Wazi, wazi kwangu?
2
Mlango hukaa wazi Watu waokolewe:
Maskini na matajiri Wa mataifa yote.
3
Maadam mlango wazi, Rafiki kaza mwendo;
Msalaba ukubali - Amana ya upendo.
4
Msalaba tutabeba Daima, na furaha!
`Pendo wa Yesu hushinda. Tunainama kwake!
- Title Mlango Wazi Key Titles undefined First Line Mlango uko wa wema, Mlango wazi huo: Author Year Composer Hymnal - Tune Metrical pattern # Stanzas Chorus Chorus Type Subjects Texts Print Texts Scripture Song