1Salama tumepita, safarini juma hii, Tumwendee Mwokozi, atubariki sasa: Siku hiyo ya raha, siku bora ya juma; Siku hiyo ya raha, siku bora ya juma. 2Utupe nuru leo toka hazina yako; Ondoa dhambi zetu, tupokee na pendo; Mikono yapumzika, tuishi ndani yako, Mikono yapumzika, tuishi ndani yako. 3Twakusanyika hapa, tusifu jina lako; Ukaribie kwetu, tupe neema Bwana; Utamu tusikize, wa raha ya milele: Utamu tusikize, wa raha ya milele: 4Injili yako leo, ishike wenye dhambi; Itupe nguvu nyingi, iponye wenye shida; Mioyo yetu shangaza, vyakula utulishe, Mioyo yetu shangaza, vyakula utulishe.