Advent Hymnals

082. NI SIKU YA FURAHA

Nyimbo Za Kristo,


1
Ni siku ya furaha, ni siku ya nuru; 
Nasi twaona raha, Kuja kushukuru; 
Leo watu wa Mungu, wadogo, wakubwa, 
Hukaribia mbingu, lilipo baraka. 

2
Leo, ndiyo bandari, nasi twawasili, 
Hiyo bustani nzuri, ya nyingi fadhili: 
Kijito cha baridi kimefanya ziwa, 
Na kiu ikizidi, twanywa maridhawa. 

3
Leo ngazi na iwe ifakayo juu, 
Mawazo na yasiwe ya duniani tu; 
Leo ni kujilisha chakula cha mbingu, 
Na kujifurahisha kwa mambo ya Mungu.



  • -
    Title Ni Siku Ya Furaha
    Key
    Titles undefined
    First Line Ni siku ya furaha, ni siku ya nuru;
    Author
    Year
    Composer
    Hymnal -
    Tune
    Metrical pattern
    # Stanzas
    Chorus
    Chorus Type
    Subjects
    Texts
    Print Texts
    Scripture Song