Advent Hymnals

090. MAPYA NI MAPENZI

Nyimbo Za Kristo,


1
Mapya ni mapenzi hayo, 
Asubuhi tuonayo; 
Saa za giza hulindwa, 
Kwa uzima kuamka. 

2
Kila saku, mapya pia, 
Rehema, wema na afya, 
Wokovu na msamaha, 
Mawazo mema, furaha. 

3
Tukijitahidi leo 
Na mwendo utupasao, 
Mungu atatueleza 
Yatakayompendeza. 

4
Mamboyetu ya dunia 
Bwana atayang'aria, 
Matata atageuza 
Yawe kwetu ya baraka. 

5
Yaliyo madogo, haya 
Bwana tukimfanyia, 
Yatosha: tutafaidi 
Huvuta kwake zaidi. 

6
Ewe Bwana, siku zote, 
Tusaidie kwa yote: 
Mwendo wetu wote vivyo, 
Uwe kama tuombavyo.




  • -
    Title Mapya Ni Mapenzi
    Key
    Titles undefined
    First Line Mapya ni mapenzi hayo,
    Author
    Year
    Composer
    Hymnal -
    Tune
    Metrical pattern
    # Stanzas
    Chorus
    Chorus Type
    Subjects
    Texts
    Print Texts
    Scripture Song