Advent Hymnals

076. MRITHI UFALME

Nyimbo Za Kristo,


1
Mrithi ufalme, kwani walala?
Karibu wokovu wasinzia?
Amka, simama, uvae silaha, 
Haraka sana, saa zapita.

2
Mrithi ufalme mbona `kawia? 
M-bona hupokei zawadi?
Haya, uvae, Mwokoziyuaja; 
Haraka, umlaki afikapo.

3
Mataifa makuu ya dunia! 
Yapigana kujiangusha;
Usisihofu dalili, mrithi; 
Ishara zote hazikawii.

4
`Sitazame anasa za dunia,
Kwani hayo yapita upesi;
Zivunje kamba zinazokufunga;
Mrithi ufalme, njoo` karudi.

5
Inua kichwa, tazama mbele tu,
M-falme aja na utukufu;
Jua laonekana milimani,
Warithi ufalme furahini.




  • -
    Title Mrithi Ufalme
    Key
    Titles undefined
    First Line Mrithi ufalme, kwani walala?
    Author
    Year
    Composer
    Hymnal -
    Tune
    Metrical pattern
    # Stanzas
    Chorus
    Chorus Type
    Subjects
    Texts
    Print Texts
    Scripture Song