1Je! Mkinzi ukutani Wa mji wa Zayuni, Habari zake usiku? Asubuhi karibu? Kuna dalili za kupambazuka? Kuna dalili za kupambazuka? 2Katika safari yetu Twaona nchi kavu? Tutalala baharini? Bandari bado mbali? Kweli, kweli tutaona ufalme? Kweli, kweli tutaona ufalme? 3Tunaona nuru yake Nyota ya asubuhi; Nyota, tukufu na safi Inang`aa mbinguni; Furahini, wokovu u karibu. Furahini, wokovu u karibu. 4Tumetazama ramani, Kweli pwani si mbali; Twende mbele, kwa upesi Tutaona bandari; Furahini, imbeni nyimbo zenu,Furahini, imbeni nyimbo zenu.