1Twendeni askari, Watu wa Mungu;Yesu yuko mbele, Tumwandame juu;Ametangulia Bwana vitani,Twende mbele kwani ndiye amini.ChorusTwendeni Askari, Watu wa Mungu; Yesu yuko mbele, Tumwandame juu;2Jeshi la shetani, likisikiaJina la Mwokozi, litakimbia; Kelele za shangwe zivume pote;Ndugu, inueni zenu sauti.3Kweli kundi dogo, watu wa Mungu,La mababa yetu ni letu fungu;Hatutengwi nao, moja imani;Tumaini moja, na moja dini.4Haya mbele watu nasi njiani,Inueni myoyo, nanyi sifuni;Heshima na sifa yake Mfalme;Juu hata chini sana zivume.