Advent Hymnals

069. CHA KUTUMAINI SINA

Nyimbo Za Kristo,


1
Cha kutumaini sina ila damu yake Bwana, 
Sina wema wa kutosha Dhambi zangu kuziosha.

Chorus
Kwake Yesu nasimama,
Ndiye mwamba: ni salama;
Ndiye mwamba: ni salama;

2
Njia yangu iwe ndefu yeye hunipa wokovu;
Mawimbi yakinipiga nguvuzake ndizo nanga.

3
Damu yake na sadaka nategemea daima,
Yote chini yakiisha Mwokozi atanitosha.

4
Nikiitwa hukumuni, Rohoni nina amani;
Nikivikwa haki yake sina hofu mbele zake.




  • -
    Title Cha Kutumaini Sina
    Key
    Titles undefined
    First Line Cha kutumaini sina ila damu yake Bwana,
    Author
    Year
    Composer
    Hymnal -
    Tune
    Metrical pattern
    # Stanzas
    Chorus
    Chorus Type
    Subjects
    Texts
    Print Texts
    Scripture Song