Advent Hymnals

055. TWAPANDA MAPEMA

Nyimbo Za Kristo,

1
Twapanda mapema na mchana kutwa 
Mbegu za fadhili hata jioni
Twangojea sasa siku za kuvuna;
Tutashangilia wenye mavuno.

Wenye mavuno wenye mavuno,
Tutasha ngilia wenye mavuno;
Wenye mavuno wenye mavuno,
Tutasha ngilia wenye mavuno.

2
Twapanda mwangani  na kwenye kivuli
Tusishindwe na baridi na pepo
Punde itaisha kazi yetu hapa
Tutashangilia wenye mavuno.

3
Twapana kwa Bwana mbegu kila siku.
Tujapoona taabu nahuzuni; 
Tuishapo shinda atatupokea:
Tutashangilia wenye mavuno.


  • -
    Title Twapanda Mapema
    Key
    Titles undefined
    First Line Twapanda mapema na mchana kutwa
    Author
    Year
    Composer
    Hymnal -
    Tune
    Metrical pattern
    # Stanzas
    Chorus
    Chorus Type
    Subjects
    Texts
    Print Texts
    Scripture Song