1Nipe Biblia nyota ya furaha, wapate nuru wasafirio;Hakuna la kuzuia amani, Kwani Yesu alituokoa.ChorusNipe Biblia neno takatifu, Nuru yako itaniongoza,Sheria na ahadi na upendo, Hata mwisho vitaendelea.2Nipe Biblia nihuzunikapo ikinijaza moyoni dhambi ;Nipe neno zuri la Bwana Yesu, Nimwone Yesu Mwokozi wangu.3Nipe Biblia nipate kuona, hatari zilizo duniani;Nuru ya neno lake Bwana Yesu, Itaangaza njia ya kweli.4Nipe Biblia taaa ya maisha; Mfariji tunapofiliwa;Unionyeshe taa ya mbinguni, Nione utukufu wa Bwana
-
Title
Nipe Biblia
Key
Titles
undefined
First Line
Nipe Biblia nyota ya furaha, wapate nuru wasafirio;