1Ninaye rafiki naye Alinipenda mbele;Kwa kamba za pendo lake Nimefungwa milele. Aukaza moyo wangu, Uache ugeuzi,Ninakaa ndani yake, Yeye Kwangu, milele.2Ninaye Rafiki ndiye, Aliyenifilia;Alimwaga damu yake, Kwa watu wote pia.Sina kitu mimi tena, Nikiwa navyo tele,Pia vyote ni amana, Ndimi wake milele.3Ninaye Rafiki naye, Uwezo amepewa;Atanilinda mwenyewe, Juu `tachukuliwa;Nikitazama mbinguni, Hupata nguvu tele;Sasa natumika chini, Kisha juu milele.4Ninaye Rafiki naye, Yuna na moyo mwema;Ni Mwalimu, Kiongozi, Mlinzi wa daima;Ni nani wa kunitenga, Na mpenzi wa mbele?Kwake nimetia nanga, ndimi wake milele.