Advent Hymnals
032. TANGU KUAMINI
Nyimbo Za Kristo,
1
Ninao wimbo mzuri, Tangu kuamini;
Wa mkombozi, Mfalme, Tangu kuamini.
Chorus
Tangu kuamini, Jina lake `tasifu,
Tangu kuamini, Nitalisifu Jina lake.
2
Kristo anitosha kweli, Tangu kuamini,
Mapenzi yake napenda, Tangu kuamini.
3
Ninalo shuhuda sawa, Tangu kuamini,
Linalofukuza shaka, Tangu kuamini.
4
Ninalo kao tayari, Tangu kuamini,
Nililorithi kwa Yesu, Tangu kuamini.
- Title Tangu Kuamini Key Titles undefined First Line Ninao wimbo mzuri, Tangu kuamini; Author Year Composer Hymnal - Tune Metrical pattern # Stanzas Chorus Chorus Type Subjects Texts Print Texts Scripture Song