1Nipe habari za Yesu, Kwangu ni tamu sana;Kisa chake cha dhamani Hunipendeza sasa.Jinsi malaika wengi walivyoimba sifa,Alipoleta amani kwa watu wa dunia.ChorusNipe habari za Yesu, Kaza moyoni mwangu;Kisa chake cha dhamani Hunipendeza sasa.2Kisa cha alivyofunga Peke yake jangwani.Jinsi alivyolishinda jaribu la shetani;Kazi aliyoifanya, Na siku za huzuni,Jinsi walivyotesa: Yote ni yaajabu!3Habari za msalaba Aliposulubishwa:Jinsi walivyomzika Akashinda kaburi.Kisa chake cha rehema. Upendo wake kwangu,Aliye toa maisha Nipokee wokovu.