Advent Hymnals

030. YESU UNIPENDAYE

Nyimbo Za Kristo,



Yesu unipendaye kwako nakimbilia,
Ni wewe utoshaye mwovu akinijia.
Yafiche ubavuni mwako maisha yangu;
Nifishe bandarini, wokoe moyo wangu.

2
Ngome nyingine sina; nategemea kwako,
Usinitupe Bwana, nipe neema yako,
Ninakuamania, kuniweshesha;
Shari wanikingia, vitani wanitosha.

3
Nakutaka mpaji, vyote napata kwako;
Niwapo muhitaji, utanijazi vyako;
Nao waangukao wanyonge wape nguvu;
Poza wauguao, uongoze vipofu.

4
Bwana umeniosha moyo kwa damu yako;
Neema ya kutosha yapatikana kwako;
Kwako Bwana naona kisima cha uzima;
Mwangu moyoni, Bwana, bubujika daima.



  • -
    Title Yesu Unipendaye
    Key
    Titles undefined
    First Line Ngome nyingine sina; nategemea kwako,
    Author
    Year
    Composer
    Hymnal -
    Tune
    Metrical pattern
    # Stanzas
    Chorus
    Chorus Type
    Subjects
    Texts
    Print Texts
    Scripture Song