1Nena rohoni Yesu, Nena kwa upoleSema kwangu kwa pendo, "Huachwi upweke."Fungua moyo wangu, Nisikie mara;Jaza roho na sifa, Sifa zako Bwana.ChorusKila siku unene, Vile kwa upole,Nong`oneza kwa pole wa pendo:"Daima utashinda, Uhuru ni wako."Nisikie maneno; "Huachwi upweke."2Nena kwa wana wako, waonyeshe njia, Wajaze kwa furaha, Fundisha kuomba;Wajifunze kutoa Maisha kamili,Wahimize ufalme, Tumwone mwokozi.3Nena kama zamani, UlipoitoaSheria takatifu: Niiweke pia;Nipate kutukuza Wewe Mungu wangu,Mapenzi yoko tena, Daima kusifu.