Advent Hymnals
007. MUNGU MSAADA WETU
Nyimbo Za Kristo,
1
Mungu Msaada wetu tangu miaka yote;
Ndiwe tumaini letu la zamani zote.
2
Kivuli cha kiti chako ndiyo ngome yetu,
Watosha mkono wako ni ulinzi wetu.
3
Kwanza havijakuwako nchi na milima,
Ndiwe Mungu; chini yako twakaa salama.
4
Na miaka elfu ni kama siku moja kwako;
Utatulinda daima, tu wenyeji wako.
5
Bwana msaada wetu tangu miaka yote,
Mlinzi wetu na ngome, daima, milele.
- Title Mungu Msaada Wetu Key Titles undefined First Line Mungu Msaada wetu tangu miaka yote; Author Year Composer Hymnal - Tune Metrical pattern # Stanzas Chorus Chorus Type Subjects Texts Print Texts Scripture Song