1
U Mtakatifu! Mungu Mwenyezi!
Alfajiri sifa zako tutaimba;
U Mtakatifu, Bwana wa huruma,
Mungu wa vyote hata milele.
2
U Mtakatifu! Na malaika
Wengi sana wanakuabudu wote;
Elfu na maelfu wanakusujudu
Wa zamani na hata milele.
3
U Mtakatifu! Ingawa giza
Lakuficha fahari tusiione,
U Mtakatifu! Wewe peke yako,
Kamili kwa uwezo na pendo.
1
Twamsifu Mungu, Mwana wa upendo,
Aliyetufia na kupaa juu.
Chorus
Aleluya! Usifiwe, Aleluya! Amin;
Aleluya! Usifiwe, utabariki.
2
Twamsifu Mungu, Roho Mtukufu,
Akatufunulia Mwokozi wetu.
3
Twamsifu Mwana, aliyetufia,
Ametukomboa na kutuongoza.
4
Twamsifu Mungu wa neema yote,
Aliyetwaa dhambi, akazifuta.
5
Twamshe tena, tujaze na pendo.
Moyoni uwashe moto wa Roho.
1
Mungu atukuzwe, kwa mambo makuu,
Upendo wake ulitupa Yesu,
Aliyejitoa maisha yake,
Tuwe nao uzima wa milele.
Chorus
Msifu, msifu, dunia sikia;
Msifu, msifu, watu wafurahi;
Na uje kwa Baba, kwa Yesu Mwana,
Ukamtukuze kwa mambo yote.
2
Wokovu kamili, zawadi kwetu,
Ahadi ya Mungu kwa ulimwengu;
Wanaomwamini na kuungama,
Mara moja wale husamehewa.
3
Alitufundisha mambo makuu,
Alihakikisha wokovu wetu;
Lakini zaidi, ajabu kubwa,
Yesu atakuja na tutamwona.
1
Jina la Yesu, salamu! Lisujidieni,
Ninyi mbinguni, hukumu, Na enzi mpeni.
Ninyi mbinguni, hukumu, Na enzi mpeni.
2
Enzi na apewe kwenu, watetea dini;
Mkuzeni Bwana wenu, Na enzi mpeni.
Mkuzeni Bwana wenu, Na enzi mpeni.
3
Enyi mbegu ya rehema nanyi msifuni;
Mmeponywa kwa neema, Na enzi mpeni.
Mmeponywa kwa neema, Na enzi mpeni.
4
Wenye dhambi kumbukeni ya msalabani.
Kwa furaha msifuni, Na enzi mpeni
Kwa furaha msifuni, Na enzi mpeni.
5
Kila mtu duniani msujudieni,
Kote-kote msifuni, Na enzi mpeni.
Kote-kote msifuni, Na enzi mpeni.
6
Sisi na wao pamoja tu mumo sifani.
Milele sifa ni moja, ni ‘enzi mpeni’.
Milele sifa ni moja, ni ‘enzi mpeni’.
1
Na tumwabudu huyo Mfalme,
Sifa za nguvu zake zivume;
Ni ngao, ni ngome, Yeye milele,
Ndizo sifa zake kale na kale.
2
Tazameni ulimwengu huu,
Ulivyoumbwa, ajabu kuu;
Sasa umewekwa pahali pake,
Hata utimize majira yake.
3
Kwa ulinzi wako, kwetu Bwana,
Twakushukuru, U mwema sana;
Hupewa chakula kila kiumbe,
Kila kitu kina mahali pake.
4
Wanadamu tu wanyonge sana,
Twakutumaini Wewe, Bwana;
Kamwe haupungui wako wema,
Mkombozi wetu, Rafiki mwema.
1
Kumekucha kwa uzuri. Nafumbua macho;
Baba amenihifadhi, Ni wake moto.
2
Bwana niwe leo kutwa, Ulinzini mwako;
Nisamehe dhambi, niwe Mikononi mwako.
3
Roho wako anikae, Moyoni daima;
Anitakase, nione Uso wako mwema.
1
Mungu Msaada wetu tangu miaka yote;
Ndiwe tumaini letu la zamani zote.
2
Kivuli cha kiti chako ndiyo ngome yetu,
Watosha mkono wako ni ulinzi wetu.
3
Kwanza havijakuwako nchi na milima,
Ndiwe Mungu; chini yako twakaa salama.
4
Na miaka elfu ni kama siku moja kwako;
Utatulinda daima, tu wenyeji wako.
5
Bwana Msaada wetu tangu miaka yote,
Mlinzi wetu na ngome, daima, milele.
1
Unisikie ninapolia, Uje, M-kombozi;
Moyo wangu hukutazamia, Uje, M-kombozi.
Chorus
Nimepotea mbali na kwangu, Nimetanga peke yangu;
Unichukulie sasa kwako: Uje, M-kombozi.
2
Sina pahali pa kupumzika, Uje, M-kombozi;
Unipe raha, nuru, uzima, Uje, M-kombozi.
3
Nimechoka, Njia ni ndefu, Uje, M-kombozi;
Macho yako kuona nataka, Uje, M-kombozi.
4
Bwana, daima hutanidharau, Uje, M-kombozi;
Kilio changu utanijibu, Uje, M-kombozi.
1
Mwumbaji, Mfalme, Vitu vyote vyako;
Ni kwa ukarimu wako; Ninabarikiwa,
Ni kwa ukarimu wako, Ninabarikiwa.
2
Uliyeniumba, Nakutegemea;
Sina budi kuzisifu Hisani zako kuu,
Sina budi kuzisifu Hisani zako kuu.
3
Nitatoa nini? Kwanza vyote vyako.
Upendo wako wadai Moyo wa shukrani,
Upendo wako wadai Moyo wa shukrani.
4
Nipewe neema, Niwe na uwezo
Wa kuishi kwako, Bwana: Siku zangu, zako,
Wa kuishi kwako, Bwana: Siku zangu, zako.
1
Kristo wa neema yote imbisha moyo wangu
Mifulizo ya baraka inaamsha shangwe kuu.
Unifunze nikupende, nikuandame kote,
Moyo wangu ukajae furaha na tumai.
2
Namshukuru sana Bwana, aniwezesha huku.
Salama aniongoza hata kule nyumbani.
Yesu alinitafuta njiani mbali kwake,
Akatoa damu yake nipone hatarini.
3
Kweli mimi mwiwa mkubwa wa neema daima;
Wema wako unifunge zaidi kwako Bwana.
Ili nisivutwe tena kukuacha, ee Mponya,
Nitwalie moyo wangu uwe wako kamili.
1
Sauti zote ziimbe, jina la Yesu li heri!
Sifa za Mfalme Mungu, jina la Yesu li heri!
Chorus
Jina li heri, jina li heri, jina la Yesu li heri.
Jina li heri, jina li heri, jina la Yesu li heri.
2
Hofu zote latuliza, jina la Yesu li heri!
Mwenye dhambi hukubali, jina la Yesu li heri.
3
Huvunja nguvu za dhambi, jina la Yesu li heri.
Damu yake hutakasa, jina la Yesu li heri.
4
Sauti yake ni tamu, jina la Yesu li heri.
Wakaburini husikia, jina la Yesu li heri.
5
Lugha maelf(u) zitaimba, “jina la Yesu li heri.
Astahili Mwana-Kondoo, jina la Yesu li heri.”
Msifu Mungu wa neema,
Enyi viumbe popote;
Wa juu pia sifuni
Baba, Mwana naye Roho!
1
Umetuahidi kwamba wawili, Watatu kwa jina lako wakija,
Utawabariki; Kwa hivi leo Twapiga magoti nyumbani pako.
Chorus
Yesu uje kwetu Utubariki;
Yesu uje kwetu Uwe karibu.
2
Umekuwa nasi siku nyingine, Tunakuhitaji mpaka mwisho.
Uje Mkombozi, tupe neema; 'Tusikie Yesu, utubariki.
3
Uje utawale sauti zetu: Nyimbo, nazo sala uziagize;
Imani izidi, ikamilike; Pendo liwe safi, na njia nuru.
1
Nitembee nawe Mungu
Alivyotembea Henok;
Mkono wangu uushike;
Unene nami kwa pole;
Ingawa njia siioni,
Yesu nitembee nawe.
2
Siwezi tembea pekee;
Pana dhoruba mbinguni;
Mitego ya miguu, elfu;
Adui wengi hufichwa;
Uitulize bahari,
Yesu nitembee nawe.
3
Ukinishika mkono,
Anasa kwangu hasara;
Kwa nguvu nitasafiri;
'Tautwika msalaba;
Hata mji wa Sayuni
Yesu nitembee nawe.
1
Nena rohoni Yesu, Nena kwa upole
Sema kwangu kwa pendo, “Huachwi upweke.”
Fungua moyo wangu, Nisikie mara;
Jaza roho na sifa, Sifa zako Bwana.
Chorus
Kila siku unene, Vile kwa upole,
Nong’oneza kwa pole wa pendo:
“Daima utashinda, Uhuru ni wako.”
Nisikie maneno: “Huachwi upweke.”
2
Nena kwa wana wako, Waonyeshe njia,
Wajaze kwa furaha, Fundisha kuomba;
Wajifunze kutoa Maisha kamili,
Wahimize ufalme, Tumwone Mwokozi.
3
Nena kama zamani, Ulipoitoa
Sheria takatifu: Niiweke pia;
Nipate kutukuza Wewe Mungu wangu,
Mapenzi yako tena, Daima 'kusifu.
1
Bwana ninakuhitaji! Ni mpofu, maskini;
Unishike mkononi, Kwako napata nguvu.
Chorus
Kila saa, Kila saa, Bwana ninakuhitaji;
Kila saa, Kila saa, Unilinde kila saa.
2
Univike na mavazi ya usikivu wako;
Nguo zangu ni machafu, Nazitamani zako.
3
Wewe ukiniongoza Nitakwenda salama;
Nenda nami siku zote, U nuru na uzima.
4
Na ikiwa m-beleni Sehemu yangu ngumu,
Au ikiwa furaha, Unilinde kila saa.
1
Si mimi, Kristo astahili sifa;
Si mimi, Kristo ajulikane;
Si mimi, Kristo katika maneno,
Si mimi, Kristo kwa kila tendo.
2
Si mimi, Kristo, kuponya huzuni;
Kristo pekee, kufuta machozi;
Si mimi, Kristo, kubeba mzigo;
Si mimi, Kristo, kupunga hofu.
3
Kristo pekee, pasipo kujisifu;
Kristo pekee, na nisizungumze
Kristo pekee, na hakuna kiburi;
Kristo pekee, sifa yangu ife.
4
Kristo pekee, mahitaji atoe
Si mimi, Kristo, kisima changu;
Kristo pekee, kwa mwili na kwa moyo;
Si mimi, Kristo, hata milele.
1
Mwokozi, kama mchunga Utuongoze leo;
Ututume malishoni; Fanya tayari boma.
Bwana Yesu, peke yako Umetuvuta kwako.
2
Tu wako, uwe rafiki, Uwe mlinzi wetu;
Kundi lako ulilinde, Tusivutwe na dhambi;
Bwana Yesu, tusike, Tukiomba, samehe.
3
Umetuahidi kwamba Utakubali watu,
Utawahurumia na Utawapa neema;
Bwana Yesu, tunapenda kuwa wako, mapema.
1
Msalabani pa Mwokozi Hapo niliomba upozi,
Moyo wangu ulitakaswa, Na asifiwe.
Chorus
Na asifiwe, Na asifiwe,
Alinikomboa kwa damu, Na asifiwe.
2
Chini ya mti msumbufu Niliomba utakatifu,
Alinikomboa kwa damu, Na asifiwe.
3
Kwa ajabu nina okoka, Yesu anakaa moyoni;
Mtini alinifia, Na asifiwe.
4
Damu ya Yesu ya dhamani Huniokoa makosani;
Huniendesha wokovuni, Na asifiwe.
1
Mungu wetu yeye mwamba, Kimbilio taabuni;
Msaada penye shida ulio karibu sana.
Chorus
Mwamba wetu kutupumzisha, yu kivuli kuburudisha
Yu Mwongozi katika njia, kimbilio taabuni.
2
Mchana usiku, yule kimbilio taabuni,
Hivyo hatutaogopa, kwani yu karibu sana.
3
Iwayo yote, Yeye tu kimbilio taabuni,
Twamjua Yeye Mlinzi aliye karibu sana.
4
Mungu wetu Ficho kwetu, kimbilio taabuni,
Siku zote uwe Boma lililo karibu sana.
1
Baba twakujia, Uwe msaada;
Uwe kimbilio, twakusihi.
Dunia ni giza tukitengwa nawe;
Tufariji hapa, Baba yetu.
Chorus
Baba twakujia, tu dhaifu,
Usitugeue, tusikie.
2
Salama tulinde, kati ya taabu;
Uwe raha yetu mashakani.
Roho yasumbuka, Baba tujalie;
Twakuomba sana, tupe nguvu.
3
Neema utupe, tukubali kwako;
Moyo wetu linda, safarini;
Tuongoe mbele, tupate kushinda
Na kufika ng’ambo, kule kwako.
1
Usinipite, Mwokozi, unisikie;
Unapozuru wengine, usinipite.
Chrous
Bwana, Bwana, unisikie;
Unapozuru wengine, usinipite.
2
Kiti chako cha rehema, nakitazama;
Magoti napiga pale, nisamehewe.
3
Sina ya kutegemea, ila wewe tu;
Uso wako uwe kwangu: nakuabudu.
4
Wewe tu u Mfariji: sina mbinguni,
Wala duniani pote, Bwana mwingine.
1
Yesu, furaha ya moyo! Hazina ya pendo, na nuru.
Yote yatupendezayo, yasilinganishwe nawe.
2
Kweli yako ya daima, wawajibu wakwitao,
Ni siku zote u mwema kwao wakutafutao.
3
U Mkate wa Uzima, kupokea ni baraka,
Twanywa kwako u kisima roho zikiburudika.
4
Mwokozi twakutamani, kwako roho hutulia;
Twakushika kwa imani, nawe watubarikia.
5
Yesu, ndiwe kwetu mwanga, tufurahishe daima;
Giza ya dhambi fukuza, uwe mwanga wa uzima.
1
Jina lake Yesu tamu Tukilisikia,
Hutupoza, tena hamu Hutuondolea.
2
Roho iliyoumia kwalo hutibika,
Chakula, njaani pia; Raha, tukichoka.
3
Jina hili ni msingi, Ngao, ngome, mwamba,
Kwa hili napata ungi, Kwangu ni akiba.
4
Yesu, Mchunga, Rafiki, Mwalimu, Kuhani,
Mwanzo, Mwisho, na Amana, Mali yangu yote!
5
Moyo wangu hauwezi Kukusifu kweli;
Ila sifa zangu hizi, Bwana, zikubali.
1
Taji mvikeni, Taji nyingi sana,
Kondoo mwake Kitini, Bwana wa mabwana;
Nami tamsifu, Alikufa kwangu,
Ni Mfalme mtukufu, Seyidi wa mbingu.
2
Taji mvikeni Mwana wa Bikira;
Anazovaa kichwani, Aliteka nyara;
Shilo wa manabii, Mchunga wa watu,
Shina na tanzu ya Yese Wa Bethilehemu.
3
Taji mvikeni Bwana wa mapenzi;
Jeraha zake ni shani, Ni vito vya enzi,
Mbingu haina hata malaika
Awezaye kuziona, Pasipo kushangaa!
4
Taji mvikeni Bwana wa Salama;
Kote-kote duniani, Vita vitakoma;
Nayo enzi yake itaendelea,
Chini ya miguu yake, Maua humea.
1
Tutokapo tubariki, Utupe kufurahi;
Tuwe na upendo wako, Neema ya kushinda;
Nawe utuburudishe Tukisarifi chini.
2
Twatoa sifa, shukurani, Kwa neno la Injili;
Matunda yake, wokovu, Yaonekana kwetu;
Daima tuwe amini, Kwa kweli yako, Bwana.
3
Siku zetu zikizidi, Tuzitoe kwa Yesu;
Tuwe na nguvu moyoni, Tusichoke njiani;
Hata tutakapoona Utukufu wa Bwana.
1
Mungu mtukufu Aliyeumba Pepo kuvuma Na radi kali;
Toa neema Unapotawala, Tupe amani, Bwana wa wema.
2
Mungu wa neema, Nchi imeacha Amri tukufu Na Neno lako;
Hasira zako Zisituharibu, Tupe amani, Bwana wa wema.
3
Mwumbaji wa haki, Watu wabaya Wamedharau Utukufu Wako;
Lakini wema wako Utadumu; Endesha kweli Bwana wa wema.
4
Tunakutolea Ibada safi Kwa ajili ya Wokovu wako;
Hivi tunaziimba Sifa zako; Wako uwezo na utukufu.
1
Tena, Mwokozi, twalitukuza
Jina lako lenye kupendeza,
Twangojea neno la amani,
Kabla hatujakwenda nyumbani.
2
Tupe amani njiani mwetu,
Wewe u mwanzo, u mwisho wetu;
Dhambini kamwe isiingie
Midomo ikutajayo wewe.
3
Utupe amani usiku huu,
Ili gizani kuwe nuru kuu.
Tulinde kwa kuwa kwako Bwana,
Usiku ni sawa na mchana.
4
Tupe amani ulimwenguni
Ndiyo dawa yetu majonzini;
Na ikitwita sauti yako,
Tupe amani milele kwako.
1
Jina lake Yesu tamu, Lihifadhi moyoni;
Litakufariji ndugu, Enda nalo popote.
Chorus
Jina la Thamani,
(Thamani) (thamani)
Tumai la dunia
Jina la thamani,
(Jina la thamani - tamu!)
Furaha ya mbinguni.
2
Jina la Yesu lafaa, Kama ngao vitani.
Majaribu yakisonga, Omba kwa jina hili.
3
Jina hili la thamani, Linatufurahisha,
Anapotukaribisha, Na tunapomwimbia.
4
Mwisho wa safari yetu, Tutakapomsujudu.
Jina hili tutasifu, Furaha ya mbinguni.
1
Yesu nakupenda, u mali yangu,
Anasa za dhambi sitaki kwangu:
Na Mwokozi aliyeniokoa
Sasa nakupenda, kuzidi pia.
2
Moyo umejaa mapenzi tele
Kwa vile ulivyonipenda mbele,
Uhai wako ukanitolea
Sasa nakupenda, kuzidi pia.
3
Ulipoangikwa msalabani,
Tusamehewe tulio dhambini;
Taji ya miiba uliyoivaa,
Sasa nakupenda, kuzidi pia.
4
Mawanda mazuri na masikani
Niyatazamapo huko mbinguni,
`Tasema na taji nitakayovaa,
Sasa nakupenda, kuzidi pia.
1
Yesu unipendaye kwako nakimbilia,
Ni wewe utoshaye mwovu akinijia.
Yafiche ubavuni mwako maisha yangu;
Nifishe bandarini, wokoe moyo wangu.
2
Ngome nyingine sina; nategemea kwako,
Usinitupe Bwana, nipe neema yako,
Ninakuaminia, mwenye kuniwezesha;
Shari wanikingia, vitani wanitosha.
3
Nakutaka Mpaji, vyote napata kwako;
Niwapo muhitaji, utanijazi vyako;
Nao waangukao wanyonge wape nguvu;
Poza wauguao, uongoze vipofu.
4
Bwana umeniosha moyo kwa damu yako;
Neema ya kutosha yapatikana kwako;
Kwako Bwana naona kisima cha uzima;
Mwangu moyoni, Bwana, bubujika daima.
1
Niimbe (niimbe) pendo lake,
Pendo la (pendo la) Yesu Bwana;
Sababu (sababu) alitoka
Kwa Baba, akafa.
Chorus
Niimbe (niimbe) pendo lake;
Sifa kuu (sifa kuu) nitatoa;
Akafa (akafa) niwe hai,
Niimbe pendo lake.
2
Machozi (machozi) alitoa,
Ijapo (ijapo) sijalia;
Maombi (maombi) yangu bado,
Aniombeapo.
3
Upendo (upendo) kubwa huo!
Dunia (dunia) haijui.
Samaha (samaha) kwa makosa,
Kubwa kama yangu.
4
Hapana (hapana) tendo jema,
Ambalo (ambalo) nilitenda,
Nataka (nataka) toka leo
Nimwonyeshe pendo.
1
Ninao wimbo mzuri, Tangu kuamini;
Wa Mkombozi, Mfalme, Tangu kuamini.
Chorus
Tangu kuamini, Jina lake `'tasifu,
Tangu kuamini, Nitalisifu jina lake.
2
Kristo anitosha kweli, Tangu kuamini,
Mapenzi yake napenda, Tangu kuamini.
3
Ninalo shuhuda sawa, Tangu kuamini,
Linalofukuza shaka, Tangu kuamini.
4
Ninalo kao tayari, Tangu kuamini,
Nililorithi kwa Yesu, Tangu kuamini.
1
Karibu sana univute, Karibu sana daima niwe.
Bwana napenda unishike, Unilinde nisitengwe nawe,
Unilinde nisitengwe nawe.
2
Karibu sana, sina kitu, Sina sadaka kwa Bwana Yesu,
Isipokuwa moyo wangu: Uutakase katika damu,
Uutakase katika damu.
3
Karibu sana, Wewe nami. Ninafurahi kuacha dhambi,
Anasa zote na kiburi: Nipe Yesu niliyemsulubi
Nipe Yesu niliyemsulubi.
4
Karibu sana, hata mwisho. Hata mbinguni nisimamapo:
Daima dawamu niwepo Nitakapoona uso wako,
Nitakapoona uso wako.
1
Nipe habari za Yesu, Kwangu ni tamu sana;
Kisa chake cha thamani Hunipendeza sasa.
Jinsi malaika wengi walivyoimba sifa,
Alipoleta amani Kwa watu wa dunia.
Chorus
Nipe habari za Yesu, Kaza moyoni mwangu;
Kisa chake cha thamani Hunipendeza sasa.
2
Kisa cha alivyofunga Peke yake jangwani.
Jinsi alivyolishinda jaribu la Shetani;
Kazi aliyoifanya, Na siku za huzuni,
Jinsi walivyomtesa: Yote ni ya ajabu!
3
Habari za msalaba Aliposulubishwa:
Jinsi walivyomzika, Akashinda kaburi.
Kisa chake cha rehema, Upendo wake kwangu,
Aliyetoa maisha, Nipokee wokovu.
1
Nimekombolewa na Yesu na sasa nimefurahi;
Kwa bei ya mauti yake mimi ni mtoto wake.
Chorus
Kombolewa! Nakombolewa na damu;
Kombolewa! Mimi mwana wake kweli.
2
Kukombolewa nafurahi, kupita lugha kutamka;
Kulionyesha pendo lake, mimi ni mtoto wake.
3
Nitamwona Mfalme wangu, katika uzuri wake;
Ambaye najifurahisha katika torati yake.
4
Najua taji imewekwa mbinguni tayari kwangu;
Muda kitambo atakuja, ili alipo, niwepo.
1
Ni siku kuu siku ile ya kumkiri Mwokozi!
Moyo umejaa tele, kunyamaza hauwezi.
Chorus
Siku kuu! Siku kuu ya kuoshwa dhambi zangu kuu!
Hukesha na kuomba tu, aniongoza miguu.
Siku kuu! siku kuu ya kuoshwa dhambi zangu kuu!
2
Tumekwisha patina, mimi mbwake, yeye mbwangu,
Na sasa nitamwandama, nikiri neno la Mungu.
3
Moyo tulia kwa Bwana, kiini cha raha yako:
Huna njia mbili tena: uwe naye, yote ndako.
1
Pendo lako , Ee Mwokozi, Hushinda pendo zote!
Kaa nasi, ndani yetu, Furaha ya mbinguni.
Yesu, u rehema tupu, Safi, na kusamehe,
Mfariji mwenye huzuni Ziondoe machozi.
2
Roho yako ya upendo Tuma kwa kundi lako;
Hebu tuirithi raha, Iliyoahidiwa.
Uondoe moyo mbaya, U Mwanzo, tena Mwisho;
Timiza imani yetu, Ilituwekwe `huru.
3
Yesu, uje kwetu sasa, Tupokee huruma;
Rudi kwetu, tena kamwe Usituache pekee.
Tungekutukuza leo, pamoja na malaika,
Imba na kutoa sifa, Ingia kwa ibada.
4
Sasa, Bwana, kazi yako, Imalize moyoni;
Takasa hekalu lako, Wokovu kamilisha!
Safisha viumbe vyako Katika wakati huu;
Tupumzike `toka dhambi, Tuingie mbinguni.
1
Nasifu shani ya Mungu, mweneza bahari,
Muumba pia wa mbingu, jua, nyota, mwezi,
Ni tukufu yako shani, mtengeza mambo
Ya nyakati na zamani, yasiyo na mwisho.
2
Kadri ya nionayo, ya kusifu Mungu;
Nchi niikanyagayo, na hayo mawingu;
Hakuna hata unyasi, usiokuza;
Na upepo wavumisha, au kutuliza.
3
Nami kwa mkono wako, naongozwa sawa,
Ni pato nikusifupokukwomba ni dawa;
Umenizingira nyuma, na mbele baraka;
Maarifa ya ajabu! Yanishinda mimi!
1
Ati, kuna mvua njema yenye neema;
Watu wanaona vyema Bwana, huninyeshei?
Chorus
Na mimi? Na mimi? Bwana, huninyeshei?
2
Sinipite, Baba mwema; dhambini nimezama:
Rehema ni za daima; Bwana hunionyeshi?
3
Sinipite, Yesu mwema; niwe nawe daima,
Natamani kukwandama: Bwana, hunichukui?
4
Sinipite, Roho mwema, Mpaji wa uzima,
Nawe shahidi wa wema, Bwana wema hunipi?
1
Njoo, Roho Mtukufu uoshe moyo wangu,
Utakase nia yangu, njoo, nijaze sasa.
Chorus
Roho Mtukufu, njoo, nijaze sasa.
Utakase nia yangu, njoo, nijaze sasa.
2
Ujalize moyo wangu Ijapo sikuoni,
Nami ninakuhitaji, njoo, nijaze sasa.
3
Nimejaa udhaifu, ninainamia kwako;
Roho Mtukufu sasa, nitilie na nguvu.
4
Unioshe, nifariji, niponye nibariki,
Unijaze moyo wangu: ndiwe mwenye uwezo.
1
Roho Mtakatifu, Kiongozi amini;
Utushike mkono Tulio wasafiri;
Utupe kusikia Sauti ya upole;
"Msafiri, fuata, Naongoza nyumbani."
2
Wewe ndiwe rafiki, Msaada karibu;
Tusoiache shakani; Nukiwa gizani
Utupe kusikia Sauti ya upole;
"Msafiri, fuata, Naongoza nyumbani."
3
Siku zetu za kazi, Zikiwa zimekwisha,
Wala hatuna tama Ila mbingu na sala:
Utupe kusikia Sauti ya upole;
"Msafiri, fuata, Naongoza nyumbani."
1
Ewe Roho wa Mbinguni, Maombi sikia!
Makao yako yafanye Mioyoni mwetu.
2
Kama nuru, tupenyeze, Giza uondoe;
Siri yako tuione, Na amani yako.
3
Kama moto, tusafishe, Choma dhambi yetu;
Roho zetu zote ziwe Hekalu la Bwana.
4
Kama umande, na uje, Utuburudishe,
Moyo `kavu utakuwa Ni wenye baraka.
5
Kama upepo Ee Roho, Katika Pente koste
Ukombozi utangaze, Kwa kila taifa.
1
Furaha gain na ushiriki, Nikimtegemea Yesu tu!
Baraka gain, tena amani, Nikimtegemea Yesu tu!
Chorus
Tegemea, salama bila hatari;
Tegemea, tegemea Mwokozi Yesu.
2
Nitaiweza njia nyembamba, Nikimtegemea Yesu tu;
Njia `tazidi kuwa rahisi, Nikimtegemea Yesu tu.
3
Sina sababu ya kuogopa, Nikimtegemea Yesu tu;
Atakuwa karibu daima, Nikimtegemea Yesu tu.
1
Hakuna rafiki kama Yesu, Hakuna, hakuna!
Tabibu mwingine wa rohoni, Hakuna, hakuna!
Chorus
Yesu ajua shida zetu; Daima ataongoza
Hakuna rafiki kama Yesu, Hakuna, hakuna!
2
Wakati ambapo hapo yeye, Hapana, hapana!
Wala giza kututenga naye, Hapana, hapana!
3
Aliye sahauliwa naye, Hakuna, hakuna!
Mkosaji asiyempenda, Hakuna, hakuna!
4
Kipawa kama Mwokozi wetu, Hakuna, hakuna!
Ambaye atanyimwa wokovu, Hakuna, hakuna!
1
Mlimani pana mwanga, Mwanga wa jua zuri
Shambani na baharini Jua tukufu liko;
Mwanga uliyo mkubwa Umo moyoni mwangu,
Kwa kuwa Yesu alipo Hapa pana mwangaza.
Chorus
Mwangaza ulio mzuri. Mwanga umo moyoni;
Akiwapo Bwana Yesu Pana mwanga moyoni.
2
Kama mavazi kikuu, Ninavua huzuni:
Nguo nzuri za kuvaa, Umenipa za kuvaa.
Nakuandama rohoni Hatanyumba ya juu
Iliyopambwa vizuri Katika pendo lako.
3
Ulinikomboa Yesu; Maisha yangu, mali,
Vyote nivyako, Mwokozi Daima nikusifu.
Nakuandama rohoni Hatanyumba ya juu
Iliyopambwa vizuri Katika pendo lako.
1
Miguuni pake Yesu, Maneno yake tamu;
Pahali palipo heri, Niwepo kila siku.
Miguuni pake Yesu, Nakumbuka upendo
Nahisani vyake kwangu, Vimenivuta moyo.
2
Miguuni pake Yesu, Hapa pahali bora
Pakuweka dhambi zangu, Pahali pa pumziko.
Miguuni pake Yesu, Hapa nafanya sala,
Kwake napewa uwezo, Faraja na nehema.
3
Unibariki Mwokozi, Ni miguuni pako,
Unitazame kwa pendo, Nione uso wako.
Nipe Bwana nia yake, Ili ionekane
Nimekaa na Mwokozi, Aliye haki yangu.
1
Ni heri kifungo Kinachotufunga,
Mioyo yetu kwa upendo Pendo la Kikristo
2
M-bele ya Baba Tunatoa sala;
Hofu, nia, masumbufu Yetu ni moja.
3
Tunavishiriki Matata na shida,
Na mara nyingi twatoa Chozi la fanaka.
4
Tunapoachana Moyoni twalia;
Lakini tutakutana M-wisho mbinguni.
1
Ninakupenda zaidi, Ya vyote vingine;
Kwani umenipa raha, Na amani, Bwana.
Chorus
Nusu haijatangazwa (tangazwa) Ya upendo wako;
Nusu haijatangazwa (tangazwa) Damu hutakasa (takasa).
2
Nakujua u karibu Kuliko dunia;
Kukukumbuka ni tamu Kupita kuimba.
3
Kweli wanifurahisha, Na nitafurahi;
Pasipo upendo wako Naona huzuni.
4
Itakuwaje Mwokozi, Kukaa na wewe,
Ikiwa ulimwenguni, Tuna furaha hii?
1
Ninaye rafiki naye Alinipenda mbele;
Kwa kamba za pendo lake Nimefungwa milele.
Aukaza moyo wangu, Uache ugeuzi,
Ninakaa ndani yake, Yeye Kwangu, milele.
2
Ninaye Rafiki ndiye, Aliyenifilia;
Alimwaga damu yake, Kwa watu wote pia.
Sina kitu mimi tena, Nikiwa navyo tele,
Pia vyote ni amana, Ndimi wake milele.
3
Ninaye Rafiki naye, Uwezo amepewa;
Atanilinda mwenyewe, Juu `tachukuliwa;
Nikitazama mbinguni, Hupata nguvu tele;
Sasa natumika chini, Kisha juu milele.
4
Ninaye Rafiki naye, Yuna na moyo mwema;
Ni Mwalimu, Kiongozi, Mlinzi wa daima;
Ni nani wa kunitenga, Na mpenzi wa mbele?
Kwake nimetia nanga, ndimi wake milele.
1
Mungu nawe nanyi daima; hata twonane ya pili,
Awachunge kwa fadhili, Mungu nawe nanyi daima.
Chorus
Hata twonane juu, hata twonane tena kwake;
Hata twonane juu, Mungu nawe nanyi daima.
2
Mungu nawe nanyi daima; awafunike mabawa,
Awalishe, awakuze; Mungu nawe nanyi daima.
3
Mungu nawe nanyi daima; kila wakati wa shida
Awalinde hifadhini; Mungu nawe nanyi daima.
4
Mungu nawe nanyi daima; awabariki na pendo
Ambalo halina mwisho; Mungu nawe nanyi daima.
1
Yesu Mwokozi, kwa hakika, Hjinipa furaha na amani;
Mrithi wa wokovu wake, Natakaswa kwa damu yake.
Chorus
Habari hiyo wimbo wangu, Daima nitamsifu Yesu.
Habari hiyo wimbo wangu, Daima nitamsifu Yesu.
2
Nijitoapo nina raha, Na kwa imani namwona Bwana;
Aniletea malaika, Wananilinda, niiokoke.
3
Hali na mali anitwaa, Katika Yesu nabarikiwa;
Nikimgoja kwa subira, Wema wake unanitosha.
1
Nipe Biblia nyota ya furaha, wapate nuru wasafirio;
Hakuna la kuzuia amani, Kwani Yesu alituokoa.
Chorus
Nipe Biblia neno takatifu, Nuru yako itaniongoza,
Sheria na ahadi na upendo, Hata mwisho vitaendelea.
2
Nipe Biblia nihuzunikapo ikinijaza moyoni dhambi ;
Nipe neno zuri la Bwana Yesu, Nimwone Yesu Mwokozi wangu.
3
Nipe Biblia nipate kuona, hatari zilizo duniani;
Nuru ya neno lake Bwana Yesu, Itaangaza njia ya kweli.
4
Nipe Biblia taaa ya maisha; Mfariji tunapofiliwa;
Unionyeshe taa ya mbinguni, Nione utukufu wa Bwana
1
Napenda kuhubiri habari ya Yesu,
Ya Bwana wa fahari na pendo zake kuu.
Kuhubiri napenda kwa hali na mali:
Mwanyewe nimeonja, najua ni kweli.
Chorus
Napenda kuhubiri kisa cha Bwana Yesu.
Ya Bwana wa fahari na pendo zake kuu.
2
Napenda kuhubirimambo ya ajabu
Na tukiya fikiri yapita dhahabu.
Kuhubiri napenda ya yaliyonifaa:
Nami sasa napenda hayo kwa kuimba.
3
Napenda kuhubiri, hunifurahisha
Tamu yake habari haiwezi kwisha.
Napenda kuhubiri wa gizani nao;
Hawana muhubiri wa kweleza chuo.
4
Kuhubiri napenda hata wajuao;
Kusikia hupenda kama wenzi wao.
Nakao kwenye fahari nikiimba wimbo.
Nitaimba habari za Mwokozi huyo.
1
Nataka nimjue Yesu, na nizidi kumfahamu,
Nijue pendo lake tu, wokovu wake kamili.
Chorus
Zaidi, zaidi, nimfahamu Yesu
Nijue upendo wake, wokovu wake kamili.
2
Nataka nione Yesu, na nizidi kusikia
Anenapo kitabuni, kujidhihirisha kwangu.
3
Nataka tena zaidi, daima kupambanua
Mapenzi yake, nifanye yale yanayompendeza.
4
Nataka nikae naye, kwa mazungumzo matamu.
Nizidi kuwaonyesha wengine wokovu wake.
1
Twapanda mapema na mchana kutwa
Mbegu za fadhili hata jioni
Twangojea sasa siku za kuvuna;
Tutashangilia wenye mavuno.
Wenye mavuno wenye mavuno,
Tutasha ngilia wenye mavuno;
Wenye mavuno wenye mavuno,
Tutasha ngilia wenye mavuno.
2
Twapanda mwangani na kwenye kivuli
Tusishindwe na baridi na pepo
Punde itaisha kazi yetu hapa
Tutashangilia wenye mavuno.
3
Twapana kwa Bwana mbegu kila siku.
Tujapoona taabu nahuzuni;
Tuishapo shinda atatupokea:
Tutashangilia wenye mavuno.
1
Walio kifoni, nenda waponye. Uwatoe walio shimoni;
Wanaoanguka uwainue; Habari njema uwajulishe.
Chorus
Walio kifoni waokoeni, Mwokozi yuko huwangojea
2
Wajapokawia anangojea Awasubiri waje tobani;
Mwokozi hawezi kuwadharau, Huwasame he tangu zamani:
3
Na ndani ya moyo wa wanadamu Huwapo shida, tena huzuni;
Lakini kwa Yesu kuna rehema Kuwaponya na kuwaokoa.
4
Walio kifoni, nenda waponye Kazi ni yetu, zawadi iko;
Nguvu kuhubiri Bwana hutoa Kwa subira tuwavute sasa.
1
Usiikatae kazi yake Bwana; Ukae tayari kuifanya kazi;
Uende po pote Mungu akwitapo,
Nawe utaona furaha kazini
Chorus
Njoo, We! Usikatae; Njoo, We! Uifanye kazi;
Usiikatae kazi yake Bwana, Ili hatimaye usikatazwe juu.
2
Usiikatae kazi yake Bwana; Kwa nini kawia? Fanya kazi leo.
Mavuno meuoe, Wachache wavuni,
Onyesha furaha Kwa kazi ya Bwana.
3
Usiikatae kazi yake Bwana; Kukataa pendo Kwako ni hatari.
Saa ya rehema, Yesu akiomba,
Ziungame dhambi, Zifutwe mbinguni.
1
Leo nina fikiria nchi nzuri Ninayotaka kuiona;
Nisimamapo karibu na Mwokozi, Tajini zitakuwa nyota?
Chorus
Sijui tajini mwangu kama nyota
Zitang`aa kila wakati!
Nitakapoamka katika majumba
Zitakuwa nyota Tajini?
2
Kwa nguvu za Bwana nitafanya kazi, Nitavuta roho za watu,
Ili niwe na nyota katika taji, Bwana anapotupa tunu.
3
Nitakuwa na furaha nikimwona, Kuweka miguuni pake
Watu walio vutwa kwa ajili ya Kazi yangu na Roho yake.
1
Fanyeni kazi zenu, usiku si mbali;
Kesheni saa zenu vumilieni;
Kwa Yesu tumikeni na hiyo injili.
Sana wahubirini watu wa mbali.
2
Fanyeni kazi zenu, giza yasongea;
Nawengi wenzi wenu wamo gizani.
Msipoteze moja dakika ni hizi:
Bwana atarejea mwisho wa kazi.
3
Fanyeni kazi zenu, hivi jua lachwa;
Wote walio kwenu apenda Mungu:
Na sisi tumjuaye tuwafundishe
Ili Yesu ajaye tumfurahishe.
1
Pengine sio milimani Utakaponiita
Pengine sio baharini Wala palipo vita;
Lakini unaponiita, Na njia siijui.
Bwana, nitajibu, ni tayari Kwanda uniagizapo.
Chorus
Ukiwa pamoja nami, Bwana, Mlimani, baharini,
Niende utakaponiita; Na fuata uendako.
2
Pengine leo kuna neno, Neno tamu la pendo,
Ambalo Yesu anataka Ninene kwa upole;
Ukiwa pamoja nami, Bwana, Nitamtafuta leo
Yele aliyepotea mbali: Nitasema upendavyo
3
Pahali pako bila shaka Pa kuvuna shambnani,
Kazi niwezayo kufanya Kwa Yesu Mkombozi;
Hivi nikikutegemea, Kwa kuwa wanipenda,
Mapenzi yako nitafanya, Na niwe upendavyo.
1
Nimemwona rafiki wa thamani kubwa,
Ananipenda kwa ‘pole, kwa pendo amini:
Kuishi kute ngwa naye, la, huki siwezi,
Tunakaa pamoja: Bwana nami.
2
Pengine nimechoka, mimi mdhaifu,
Ndipo ninamtegemea, alivyoalika;
Huniongoza njiani, pahali pa nuru,
Twatembea pamoja: Bwana nami.
3
Namweleza huzuni, na fura ha yangu,
Vile ninavyosumbua, vinavyopendeza;
Huniagiza kutenda, yanayonipasa,
Twazungumza pamoja: Bwana nami.
4
Ajua natamani, kuwavuta watu,
Hivyo ananipeleka, kutangaza Neno;
Nitangaze pendo lak, kwa niniakafa;
Twahubiri pamoja: Bwana nami.
1
Napenda kitabu chake, kilichotoka mbinguni,
Barua kwangu ya Bwana Ujumbe wake wa`pendo.
2
Humo ndani ya kitabu Sura ya Yesu naona;
Karatasi zimekuwa, Wayo zake za Mwongozi.
3
Mapenzi yake Mwumbaji, Kubwe la asali tamu;
Natamani kuuonja, Ule mkate wa uzima.
4
Mapenzi Yake Mwumbaji, Yanafunuliwa humo;
Hazina kuu ya hekima, Utajiri wa ajabu.
5
Mwangaza wa ulimwengu Angaza humo moyoni!
Uwe mwandamizi pote, Taa ya hatua zangu.
1
Niuonapo msalaba, Kristo aliponifilia;
Kwangu pato ni hasara. Kiburi nakichukia.
2
Na nisijivune, Bwana, Ila kwa sadaka yako;
Upuzi sitaki tena, Zi chini ya damu yako.
3
Tangu kichwa hata nyayo, Zamwagwa pendo na hamu,
Ndako pweke hamu hiyo. Pendo zako zimetimu.
4
Vitu vyote vya dunia, Si sadaka ya kutosha;
Pendo zako zaniwia, Nafsi, mali, na maisha.
1
Piga panda ya Injili, onyesha watu wote;
Ili anayesikia atubu, aokoke.
Chorus
Piga panda ya Injili, upige kwa nguvu;
Mungu amekuagiza mateka wawe huru.
2
Upige vilimani, kwa kila tambarare;
Pande zote, miji yote isikie Injili.
3
Uipige mipakani, barabarani pia;
Iwatangazie wote, wanakwitwa na Baba.
4
Uipige! Watu wengi wataka wawe huru;
Waambie kwamba Yesu asema "Njoni kwangu."
1
Twendeni askari, Watu wa Mungu;
Yesu yuko mbele, Tumwandame juu;
Ametangulia Bwana vitani,
Twende mbele kwani ndiye amini.
Chorus
Twendeni Askari, Watu wa Mungu;
Yesu yuko mbele, Tumwandame juu;
2
Jeshi la shetani, likisikia
Jina la Mwokozi, litakimbia;
Kelele za shangwe zivume pote;
Ndugu, inueni zenu sauti.
3
Kweli kundi dogo, watu wa Mungu,
La mababa yetu ni letu fungu;
Hatutengwi nao, moja imani;
Tumaini moja, na moja dini.
4
Haya mbele watu nasi njiani,
Inueni myoyo, nanyi sifuni;
Heshima na sifa yake Mfalme;
Juu hata chini sana zivume.
1
Roho yangu amka sasa, mara jitahidi;
Shindano ni lake Bwana, zawadi ni taji.
2
Sauti ni yake Mungu inayokuita;
Ndiyo aliyekirimu taji ya uzima.
3
Mashaidi ndio wengi wanao kuona;
Ya nyuma usifikiri bali mwendo kaza.
4
Bwana umetuanzisha katika shindano;
Kwa vile tunaposhinda ushindi ni wako.
1
Kesha roho yangu, adui maelfu
Hujaribu kuangusha, kuvuta dhambini.
2
Ukeshe, uombe, ili ushindwe;
Fanya vita kila siku, omba msaada.
3
Kushinda ni bado: ulinde silaha;
Usiache kupigana hata una taji.
1
Umtetee Mungu duniani ijapo pepo kali za vuma;
Mwambani pekee pana nguvu Dhambi ikimea.
Chorus
Tusimame imara katika mwamba,
Mwamba wa Kristo pekee;
Ndipo salamini tutasimama
Kule kitini pa enzi.
2
Itetee haki kwa bidii, kwa moyo mnyofu wa imani;
Mwambani pekee utashinda wingi wa upotovu.
3
Itetee kweli, itadumu, ijapo kawia itashinda;
Mwambani pekee pana raha yaishapo tufani.
1
Cha kutumaini sina ila damu yake Bwana,
Sina wema wa kutosha Dhambi zangu kuziosha.
Chorus
Kwake Yesu nasimama,
Ndiye mwamba: ni salama;
Ndiye mwamba: ni salama;
2
Njia yangu iwe ndefu yeye hunipa wokovu;
Mawimbi yakinipiga nguvuzake ndizo nanga.
3
Damu yake na sadaka nategemea daima,
Yote chini yakiisha Mwokozi atanitosha.
4
Nikiitwa hukumuni, Rohoni nina amani;
Nikivikwa haki yake sina hofu mbele zake.
1
Wapenzi wa Bwana ije raha yenu! Imbeni nyimbo za raha,
Imbeni nyimbo za raha; Za ibada yenu, za ibada yenu.
Chorus
Twenenda Zayuni, mji mzuri Zayuni!
Twenenda juu Zayuni, Ni maskani ya Mungu.
2
Wasiimbe wao wasioamini, Watoto wa Mungu ndio,
Watoto wa Mungu ndio, Waimbao chini, waimbao chini,
3
Twaona rohoni baraka za Mungu, Tusijafika mbinguni,
Tusijafika mbinguni, Kwenye utukufu, kwenye utukufu.
4
Tutakapomwona masumbuko basi, Huwa maji ya uzima,
Huwa maji ya uzima,Anasa halisi, anasa halisi.
1
Kesha ukaombe panapo mafasi;
Wakati si mwingi, Kwa vile ukeshe
Mwili ni dhaifu, Adui hodari
karibu atakuja, Bwana wa arusi.
Chorus
Kesha, Omba, Kesha, Omba,
Kesha Kaombe gizani, mchana,
Daima kesha.
2
Fukuza usingizi, fukuza mashaka;
Ahadi ni yako, raha ya milele
Bwana alkesha kwa ajili yako;
Jasho yeke ikawa matone ya dame.
3
Yesu umkubali awe nguvu zako;
Silaha uzivae; adui karibu.
Sasa nafasi iko, isipite bure;
Bila kukawia masihiya kesha.
1
Tuta jenga juu ya Mwamba Wa Yesu, Mwaba wa kale;
Tutavumilia kishindo Tufani ivumapo.
Chorus
Tuta jenga juu, ( tutajenga juu ya Mwamba mkuu)
Tuta jenga juu, ( tutajenga juu ya Mwamba mkuu)
Tutajenga juu ya Mwamba mkuu, Juu yake yesu.
2
Wengine hujenga katika Mchanga wa ulimwengu;
Wengine katika mawimbi Ya anasa za dhambi.
3
Jenga nawe juu ya mwamba, Msingi pekee wa kweli:
Tumai lake litadumu, Tumai la wokovu.
1
Nakaza mwendo mbinguni, kila siku napanda juu;
Naomba nikisafiri, "Bwana uniongoze juu."
Chorus
Bwana uniinue juu Kwa imani hata mbingu.
Juu kuliko dunia; Bwana uniongoze juu.
2
Moyo wangu hautaki Kukaa palipo shaka;
Wengine wapenda chini Nia yangu ni kupanda.
3
Nataka kupanda juu Nisishindwe na adui;
Kwa imani nasikia Sauti ya washindaji.
4
Kupanda juu nataka Niuone utukufu;
Hata mwisho nitaomba, "Bwana uniongoze juu."
1
Niambie, Ee mlinzi, Umepambazuka je!
Utukufu wa Zayini, Pana dalili zake?
Msafiri uondoke, Utazame mbinguni,
Kiunoni ujifunge, Ni kucha alfajiri.
2
Mlinzi inamulika Nuru njiani mwako,
Dalili za kuja kwake, Kwamba siku karibu;
Panda itakapolia Itawaamsha wafu,
Watakatifu wa Mungu, Kuwapa kutokufa.
3
Mlinzi, ione nuru Ya mwaka wa Sabato;
Sauti zinatangaza Ufalme ni karibu;
Msafiri ninaona Mlima wa Zayuni,
Mji wa Yerusalemi Nayo fahari yake.
4
Kwenye mji wa dhahabu Anaketi mfalme
Katika kiti kizuri: huku anatawala.
Pana amani po pote, Mashamba husitawi;
Na ardhi ina rutuba; Mito ni mitulivu.
5
Mlinzi, twaribia Nchi iliyo nzuri;
Twende mbele, tufurahi, Nchi inachangamka,
Sikieni kuna wimbo Wa waliookoka;
Kaza mwendo, Ujiunge Na kundi Kubwa hili.
1
Msingi imara, ninyi wa Bwana,
Umewekwa kwenu kwa neno lake.
Nini zaidi atasema Bwana,
Imaniyenu ipate kuzidi?
2
Wambiwapo vuka maji ya giza,
Mito ya mashaka haitazidi;
`Takuwapo nawe, nikuwezeshe,
Shida upatazo zisikutishe!
3
Utakapopishwa ndani ya moto
Nguvu nitakupa, upate pato;
Huteketezwi, ila taka zako.
Nazitasalia dhambi zako.
4
Na mtu aliye nitegemea
Nguvu za Jehanamu zijapotisha,
Kamwe kwa adui sitamtia;
Mtu wangu kamwe sitamwacha.
1
Mrithi ufalme, kwani walala?
Karibu wokovu wasinzia?
Amka, simama, uvae silaha,
Haraka sana, saa zapita.
2
Mrithi ufalme mbona `kawia?
M-bona hupokei zawadi?
Haya, uvae, Mwokoziyuaja;
Haraka, umlaki afikapo.
3
Mataifa makuu ya dunia!
Yapigana kujiangusha;
Usisihofu dalili, mrithi;
Ishara zote hazikawii.
4
`Sitazame anasa za dunia,
Kwani hayo yapita upesi;
Zivunje kamba zinazokufunga;
Mrithi ufalme, njoo` karudi.
5
Inua kichwa, tazama mbele tu,
M-falme aja na utukufu;
Jua laonekana milimani,
Warithi ufalme furahini.
1
Je! Mkinzi ukutani
Wa mji wa Zayuni,
Habari zake usiku?
Asubuhi karibu?
Kuna dalili za kupambazuka?
Kuna dalili za kupambazuka?
2
Katika safari yetu
Twaona nchi kavu?
Tutalala baharini?
Bandari bado mbali?
Kweli, kweli tutaona ufalme?
Kweli, kweli tutaona ufalme?
3
Tunaona nuru yake
Nyota ya asubuhi;
Nyota, tukufu na safi
Inang`aa mbinguni;
Furahini, wokovu u karibu.
Furahini, wokovu u karibu.
4
Tumetazama ramani,
Kweli pwani si mbali;
Twende mbele, kwa upesi
Tutaona bandari;
Furahini, imbeni nyimbo zenu,
Furahini, imbeni nyimbo zenu.
1
Mpaka lini Bwana, Utakaa mbali?
Kumetuchosha moyo kukawia hivi.
Utatujia lini, Ili tufurahi
Katika ile nuru, kuja kutukufu?
2
Mpaka lini Yesu, Utaacha watu
Uliowakomboa, Wawe na mashaka?
Wachache waamini, Kwamba utarudi;
Wachache wa tayari, Bwana kukulaki.
3
Waamshe watu wako, Tangaza kilio:
"Mwe watakatifu, Bwanayu karibu!"
Utatujia lini, Ili tufurahi
Katika ile nuru, Kutukufu?
1
Nataka Imani hii: Imani imara,
Ambayo haitetemi Kitu chote
Wakati wa shida,
Wakati wa shida.
2
Isiyonung`unika Huzuni, taabu;
Lakini katika saa ya matata
Humwamini Mungu,
Humwamini Mungu.
3
Imani inayo ng`aa katika tufani;
Isiyoogopa giza, wala shida,
Njaa na Hatari,
Njaa na hatari.
4
Haiogopi dunia, Kudharau kwake;
Haiangushwi na hila, na uwongo
Dhambi na ogofyo,
Dhambi na ogofyo.
5
Bwana, nipe imani hii, Hivi nitaweza
Kuonja hapa chini ulimwenguni,
Kurithi furaha,
Kurithi furaha.
1
Tupe moto wa uhai Uliowaka zamani,
Uliowaongoza juu Wazee watakatifu.
2
Wapi roho iliyokaa Moyoni mwa Ibrahimu?
Kadhalika ndugu Paulo Aliwezeshwa na moto.
3
Neema yako haina Nguvu siku hizi sawa
Kama wakati wa Musa, Ayubu na wa Eliya?
4
Zamani za kale, Bwana, Kumbuka na kwa rehema,
Zihuishe roho zetu Kwa Roho Mtakatifu.
1
Siku sita zimepita, Sabato tena karudi;
Shangilie roho yangu, itukuze kwa busara.
2
Msifuni awapaye pumziko tamu wachovu,
Kwake roho yatulizwa, kupita siku nyingine.
3
Moyo wetu ufurahi, na kutoa mashukuru;
Ujalizwe raha ile, yasipitikwa kamwe.
4
Raha hiyo ya rohoni, ni amana ya pumziko
Ambalo limewekwa juu, kikomo cha masumbuko.
1
Ni siku ya furaha, ni siku ya nuru;
Nasi twaona raha, Kuja kushukuru;
Leo watu wa Mungu, wadogo, wakubwa,
Hukaribia mbingu, lilipo baraka.
2
Leo, ndiyo bandari, nasi twawasili,
Hiyo bustani nzuri, ya nyingi fadhili:
Kijito cha baridi kimefanya ziwa,
Na kiu ikizidi, twanywa maridhawa.
3
Leo ngazi na iwe ifakayo juu,
Mawazo na yasiwe ya duniani tu;
Leo ni kujilisha chakula cha mbingu,
Na kujifurahisha kwa mambo ya Mungu.
1
Ewe skuli ya Sabato,
U pazuri sana;
Moyo wangu wanivuta,
Nije kwako leo.
Chorus
Sabato . . . ni nzuri . . .
Sabato . . . ni nzuri . . .
Moyo wangu wanivuta,
Nije kwako leo.
2
Moyo wangu mpotovu,
Hapa una raha;
Ndipo nimwonapo Yesu,
Nije kwako leo.
3
Hapa Yesu mwenye pendo
Aniita pole:
Nimtolee moyo Yeye,
Nije kwako leo.
1
Ikumbuke kote Sabato ya Bwana,
Siku tamu na bora, kupita nyingine;
Yatuletea raha, na furaha kweli,
Mwanga wake hungaza, urembo wa Yesu.
Chorus
Karibie, karibie, Sabato tamu;
Karibie, Yesu pia, Bwana wa raha.
2
Itakase kweli, ukamsifu leo,
Yeye aliye sema "Mimi ndiye njia";
Nasi tukimfuata mkombozi hapa.
Atatunywesha tele maji ya uzima.
3
Siku ya nderemo! Tupishe wakati,
Tukimwimbia Yesu Rafiki Mpendwa;
Mponya wetu leo, U mwema ajabu!
Ukae kwetu, Bwana, moyoni daima.
1
Salama tumepita, safarini juma hii,
Tumwendee Mwokozi, atubariki sasa:
Siku hiyo ya raha, siku bora ya juma;
Siku hiyo ya raha, siku bora ya juma.
2
Utupe nuru leo toka hazina yako;
Ondoa dhambi zetu, tupokee na pendo;
Mikono yapumzika, tuishi ndani yako,
Mikono yapumzika, tuishi ndani yako.
3
Twakusanyika hapa, tusifu jina lako;
Ukaribie kwetu, tupe neema Bwana;
Utamu tusikize, wa raha ya milele:
Utamu tusikize, wa raha ya milele:
4
Injili yako leo, ishike wenye dhambi;
Itupe nguvu nyingi, iponye wenye shida;
Mioyo yetu shangaza, vyakula utulishe,
Mioyo yetu shangaza, vyakula utulishe.
1
Ukaribie tena, ewe siku ya raha;
Roho yakusalimu kama mwanga wa mbingu.
2
Raha yako tulivu, yafurahisha moyo;
Yatuliza taabu, hata waisha mwendo.
3
Ee siku takatifu, sifa na maombi,
Na kutuhekimisha, baraka yako kubwa.
1
Siku ya Sabato, siku takatifu,
Watu wako Mungu wetu, waipenda sana.
2
Ulitakasa, uliibariki,
Siku hiyo ya Sabato, siku yako Bwana.
3
Nasi tubariki tukikuabudu,
Katika siku ya raha, siku yako Bwana.
4
Halafu mbinguni, pamoja na Wewe.
Tunataka kuzishika Sabato za Bwana.
1
Siku hii ya Sabato, Tamu kufikiri
Juu ya Mungu na Mbingu Kuacha dunia.
2
Tamu kusikia Neno Toka mhubiri
Anayefundisha toba, Tupate uzima.
3
Katika vita na dhambi, Ikiwa twashindwa,
Yeye atatupa nguvu Aonaye moyo.
1
Bwana asubuhi kucha nitakuinua
Sauti yangu kuomba, nipate baraka.
2
Nakuomba roho yako niongozwe nayo;
Nifanye yanipasayo, na mapenzi yako.
3
Wanaokutegemea, U Mlinzi wao;
Matumaini wanayo, utayatimiza.
4
Na kwa wingi wa fadhili, Nyumbani mwako juu
Nitaingia na wimbo, Pale kusujudu.
1
Mapya ni mapenzi hayo,
Asubuhi tuonayo;
Saa za giza hulindwa,
Kwa uzima kuamka.
2
Kila saku, mapya pia,
Rehema, wema na afya,
Wokovu na msamaha,
Mawazo mema, furaha.
3
Tukijitahidi leo
Na mwendo utupasao,
Mungu atatueleza
Yatakayompendeza.
4
Mamboyetu ya dunia
Bwana atayang'aria,
Matata atageuza
Yawe kwetu ya baraka.
5
Yaliyo madogo, haya
Bwana tukimfanyia,
Yatosha: tutafaidi
Huvuta kwake zaidi.
6
Ewe Bwana, siku zote,
Tusaidie kwa yote:
Mwendo wetu wote vivyo,
Uwe kama tuombavyo.
1
Kaa nami, ni usiku tena;
Usiniache gizani, Bwana;
Msaada wako haukomi;
Nili peke yangu kaa nami.
2
Siku zetu hazikawi kwisha;
Sioni la kunifurahisha;
Hakuna ambacho hakikomi;
Usiye na mwiso, kaa nami.
3
Nina haja nawe kila saa;
Sina mwingine wa kunifaa;
Mimi nitaongozwa na nani
Ila wewe Bwana, kaa nami.
4
Sichi neno uwapo karibu;
Nipatalo lote si taabu;
Kifo na kaburi haviumi;
Nitashinda kwako kaa nami.
5
Nilalapo nikuone wewe,
Gizani mote nimulikiwe;
Nuru za mbinguni hazikomi;
Siku zangu zote kaa nami.
1
Magharibi jua limekwisha kushuka,
Mwezi na nyota sasa vinamsifu Muumba wa usiku
Chorus
Mungu Mtukufu, Mungu Mkuu,
Wote juu mbinguni, na wanadamu chini Twakusifu.
2
Mpaji wa uhai, ukaaye mbinguni.
Utuifadhi sisi, tufahamu gizani, U karibu.
3
Mapenzi yako makuu yawe nasi usiku,
Tuli usingizini, kucha vivyorohoni tushukuru.
4
Na utakapo kuja na nguvu kutawala,
Mungu wangu kubali kunichukua mimiulko juu.
Baba, Mwana, Roho, Mungu wetu,
Wote juu mbinguni, na wanadamu chini twakusifu.
1
Jua la rohoni mwangu, mpendwa Mwokozi wangu;
Usiku giza hapana, ukiwa karibu Bwana
2
Nikipata usingizi, nijaze fikira hizi,
Nitamu sana, nilale pendoni mwako milele.
3
Kaa nami, ewe Bwana, usiku kama mchana,
Nisiishi mbali nawe; ni uhai kuwa nawe.
4
Kama mtotomnyonge ameshawishwa atange,
Mtafute Ewe Bwana, ujirudishie tena.
5
Wagonjwa wape amani, waneemeshe maskini,
Waliao, Mtulizi, wape wote usingizi.
6
Asubuhi tutokapo, tukaribie tulipo;
Twingiapo duniani tuwe mwako mkononi.
1
Popote mashamba yajaa tele nafaka pevu,
Popote yang`aa meupe bondeni na nyandani.
Chorus
Mwenye mavuno twasihi upeleke wavuni,
Wayakusanye mazao, hata kazi yaishe.
2
Wapeleke uchaoni, waende na jotoni,
Hata jua lishukapo wakusanye ko kote.
3
Enyi wakazi wa Bwana yaleteni mazao,
Na jioni ingieni kwake na furaha kuu.
1
Sikieni neno la Mungu wetu, zileteni zaka kwa hazina
Leteni na mioyo yenu yote; mibaraka itakuja.
Chorus
Zileteni zaka kwa hazina, kanijaribu sasa nazo;
Nitakupeni mibaraka, zaidi ya nafasi ya kupewa.
2
Wakati Roho Mtakatifu kwako? Uzilete zaka kwa hazina
Ukae karibu na Bwana wako, ndipo utabarikiwa.
3
Je,una kasoro na Bwana wako? Uzilete zaka kwa hazina,
Uzilete kama alivyo sema, Ndipo utabarikiwa.
4
Ushukuru Bwana na moyo wote, unapo leta zaka ghalani;
Usadiki ahadi zake zote, ndipo utabarikiwa.
5
Tuimbe sote nyimbo za furaha, tunapoleta zaka ghalani
Twimbe kabisa na furaha kubwa, kwani tutabarikiwa.
1
Mali yako sasa, Bwana, tutatoa;
Hatuna yaliyo yetu, Yote ni vipaji.
2
Sisi watumishi, Twaungama deni;
Tungeirudisha kwake, Iliyo ya Bwana.
3
Utusaidie, Upendo kujua,
Kwa ajili yao wote Walio gizani.
4
Neno tumaini Na tegemea:
Kwamba lote tufanyalo, Tulifanye kwako.
1
Sioshwi dhambi zangu? Bila damu yake Yesu,
Hapendezewi dhambi zangu? Bila damu yake Yesu.
Chorus
Hakuna kabisa Dawa ya makosa
Ya kututakasa ila Damu yake Yesu.
2
La kunisafi sina, Ila Damu yake Yesu.
Wala udhuru tena, ila Damu yake Yesu.
3
Sipati patanishwa, Bila damu yake Yesu,
Hukumu yanitisha, Bila damu yake Yesu.
4
Sipati tumaini, Bila damu yake Yesu,
Wema wala amani Bila damu yake Yesu.
5
Yashinda ulimwengu, Iyo, damu yake Yesu,
Na kutufikisha juu, Iyo, damu yake Yesu.
1
Nilikupa wewe, damu ya moyoni,
Ili wokolewe, winuke ufuni.
Chorus
Nimekunyima ni wewe? Umenipa nini?
Nimekunyima ni wewe? Umenipa nini?
2
Nilikupa miaka yangu duniani;
Upate inuka, kuishi mbinguni.
3
Nimekuiletea, huku duniani;
Pendo na wokovu, zatoka mbinguni.
4
Nipe siku zako, udumu mwangani;
Na taabu yako, wingie rahani.
Nafsi, nafsi, pendo, mali, twae Imanweli.
Nafsi, nafsi, pendo, mali, twae Imanweli.
1
Twende kwa Yesu mimi nawe, Njia atwonya tuijue
Imo Chuoni na mwenyewe, Hapa asema, njoo!
Chorus
Na furaha tutaiyona, Mioyo ikitakata sana,
Kwako Mwokozi kuonana, Na milele kukaa.
2
"Wana na waje," atwambia, Furahini kwa kusikia;
Ndiye Mwokozi wetu hasa, Na tumtii, njoni.
3
Wangojeani? Leo yupo; Sikiza sana asemapo;
Huruma zake zitwitapo, Ewe kijana, njoo.
1
Kuwatafuta wasioweza, Kuomba wamrejee Yesu,
Kuwaambia maneno yake, "Njooni kwangu, nawapenda".
Chorus
Nitakwenda (Nitakwenda) niwatafute
Wapotevu (wapotevu) wageuke,
Waingie (Waingie) Katika zizi
La Mwokozi (La Mwokozi) Yesu Kristo
2
Kuwatafuta wasioweza, Waonyeshwe Mwokozi wetu;
Kuwaongoza, wapate wote uzima ule wa milele.
3
Kazi hiyo nataka kufanya, Leo nimesikia mwito;
Kuwainua waangukao, waletwe kwake yesu Njia.
1
Yesu Akwita, Akwita wewe, Uje leo, uje leo,
Kwani kusita, akwita wewe, Unatanga upeo.
Chorus
Msiskie, msikie,
Yesu akwita, ujitoe moyo sasa.
2
Waliochoka, na wapumzike, Uje leo, uje leo,
Wenye mizigo, wenye huzuni, Wapate mapumziko.
3
Anakungoja uliye yote, Uje leo, uje leo,
Uliyekosa, usijifiche: Woshwe, uvikwe nguo.
4
Yesu asihi wakawiao, Waje leo, waje leo,
Watafurahi waaminio; Amka, upesi, Njoo.
1
Mlangoni pa moyo; Mgeni! (Amesimama)
Amesimama pale, Mgeni! (Amesimama)
Umkaribishe sasa,
Umkaribishe Mwana
Wa Baba wa upendo: Mgeni! (Umkaribishe)
2
Moyo wako kwa Bwana, Fungua. (Fungulieni)
Asikuache mbali, Fungua. (Fungulieni)
Umkubali Rafiki,
Roho atafariji
Naye atakutunza: Fungua. (Fungulieni)
3
Usikie sauti Ya Bwana. (Uisikie)
Uyachague mambo Ya Bwana. (Mambo ya Bwana)
Ufungue mlango,
Usimwambie bado:
Jina lake tumai---- Yu Bwana. (Jina la Bwana)
4
Na ufungue moyo, Kwa Bwana (Fungulieni)
Utapewa msaada, Wa Bwana (Msaada wetu)
Uzuri utavikwa
Dhambi ataondoa,
Ukifungua moyo. Kwa Bwana (Fungulieni)
1
Yesu huita kwa upole mwingi, atwita wewe nami; Moyoni mwetu hungoja,
hukesha, Hukungojea wewe.
Chorus
"Njoni kwangu, Mliochoka, njoni: Yesu huita kwa upole mwingi, Akwita,
"uje kwangu"
2
Atuombeapo usikawie, Hutuombea sisi; Usidharau wema ma huruma, Huruma
kwetu sisi.
3
Siku za maisha hupita hima, Hupita kwako, kwangu; Usiku waja, kifo
kinakuja, Huja kwako na kwangu.
4
Fikiri juu ya upendo wake, Upendo kwako, kwangu; Dhambi zetu amekwisha
samehe. Masamaha ni yetu.
1
Yesu aliniita, "Njoo, Raha iko kwangu,
Kichwa chako ukilaze kifuani mwangu."
Nilikwenda kwake mara, Sana nilichoka;
Nikapata kwake raha na furaha tena.
2
Yesu aliniita, "Njoo, Kwangu kuna maji:
Maji ya Uzima, bure, unywe uwe hai."
Nilikwenda kwake mara Na maji nikanywa:
Naishi kwake na kiu kamwe sina tena.
3
Yesu aliniita, "Njoo, Dunia i giza,
Ukinitazama, nuru `Takungarizia."
Nilikwenda kwake mara, Yeye jua langu,
Ni kila wakati mwanga safarini mwangu.
1
Mchungaji mpenzi hukuita uje
Katika zizi lake panapo salama;
Akina wanawake, waume vijana,
Yesu aliye kweli, huwaita kwake.
Chorus
Huita kwa moyo wa huruma, "Uliyepotea uje kwangu"
Hivi kukungoja anadumu, Bwana Yesu Mchunga.
2
Akatoa maisha kwa ajili yetu;
Ataka wapotevu waje kwake sasa;
Tusijihatirishe; Kwake tu salama;
Sikia wito wake, Mchungaji wetu.
3
Tusikawie tena, adui Shetani,
Kama mbwa wa mwitu, atatuharibu;
Tunaitwa na Yesu, Mkombozi wetu,
Tuingie zizini, panapo nafasi.
1
Ukitafuta mali, Huna wasaa kwa Yesu?
Kwa matendo ya haki Huna wasaa kwa Yesu?
Anasa za dunia, Mambo yako ya raha
Haya unatafuta; Huna wasaa kwa Yesu?
2
Mambo yanakusonga: Kwakehuna nafasi?
Watekwa na dunia, Kwake huna nafasi?
Humwona m-langoni, Anapopiga hodi?
Daima hukusihi: Kwake huna nafasi?
3
Sa-a ni za thamani, Kwake hamnayo kazi
Wala hamfanyi bidii, Kwake hamnayo kazi?
Hamkufikia kwao Waliomo shimoni
Na waliopotea? Kwake hamnayo kazi?
4
Na wazaa majani tu? Huna tunda kwa Yesu?
Mikono I mitupu, Huna tunda kwa Yesu?
Huna chembe kwa ghala Kazi yako kulipa;
Wala huna furaha Unapomwona Yesu?
1
Sauti ni yake Bwana, "Kwenda nani tayari?"
Mavuno yanakawia, Nani atayavuna?
Kwa kudumu anaita, Zawadi atatoa;
Nani atakayejibu, "Nipo Bwana nitume."
2
Kama huwezi safari, Hata nchi za mbali,
Pana watu karibuni, Wasiomjua Yesu;
Kama huwezi kusema, Jinsi ya malaika,
Waweza kuutangaza, Upendo wa Mwokozi.
3
Ingawa huwezi kuwa, Mkesha mlangoni,
Ukiwatolea watu, Nafasi ya uzima;
Kwa sala na kwa sadaka, Watoa msaada,
Kama Harun mwaminifu, Kuinua mikono.
4
Roho za watu zikifa, Bwana akikuita,
Usiseme kwa uvivu, "Hakuna kazi kwangu".
Kwa furaha anza kazi, Ile aliyokupa,
Ukajibu mara moja, "Nipo Bwana nitume".
1
Tumesikia mbiu: Yesu huokoa; Utangazeni kote, Yesu huokoa.
Tiini amri hiyo: nchini baharini. Enezeni mbiu hii: Yesu huokoa.
2
Imba nawe askari: Yesu huokoa Kwa nguvu ya kombozi, Yesu huokoa.
Imbeni wenye shida, unapoumwa moyo, Na kaburini imba: Yesu huokoa.
3
Mawimbini uenee. Yesu huokoa; Wenye dhambi jueni: Yesu huokoa;
Visiwa na viimbie, vilindi itikeni, Na nchi shangilie: Yesu huokoa.
4
Upepo utangaze: Yesu huokoa; Mataifa yashangaa: Yesu huokoa.
Milimani, bondeni, sauti isikike Ya wimbo wa washindi: Yesu huokoa.
1
Anisikiaye, aliye yote, sana litangae, wajue wote,
Duniani kote neno wapate, atakaye na aje!
Chorus
Ni "atakaye," ni "atakaye"; Pwani hata bara, na litangae:
Ni Baba mpenzi alinganaye atakaye na aje.
2
Anijiliaye, Yesu asema, asikawe, aje hima mapema;
Ndimi Njia, kweli, ndimi uzima: atakaye na aje!
3
Atakaye aje, ndiyo ahadi; atakaye hiyo haitarudi!
Atakaye lake, ni la ahadi! Atakaye na aje.
1
Mlango uko wa wema, Mlango wazi huo:
Yesu ameufungua Na hakuna kufunga
Chorus
Mlango wazi, ajabu, Uliachwa wazi kwangu?
Kwangu, Kwangu? Wazi, wazi kwangu?
2
Mlango hukaa wazi Watu waokolewe:
Maskini na matajiri Wa mataifa yote.
3
Maadam mlango wazi, Rafiki kaza mwendo;
Msalaba ukubali- Amana ya upendo.
4
Msalaba tutabeba Daima, na furaha!
`Pendo wa Yesu hushinda. Tunainama kwake!
1
Tabibu mkuu huyu, Yesu mwenye huruma
Atuletaye faraja: Yesu, Mwokozi wetu.
Chorus
Imbeni, Malaika, SIfa za Bwana wetu:
Jina la pekee kwetu, ni la Yesu Bwana.
2
Mwana Kondo-o msifuni Mwokozi;
Hatia zote na dhambi, Huziondoa Yesu.
3
Hakuna jina jingine, Linalofa-a sifa;
A-u kutufurahisha, Isipokuwa lake.
4
Naye atakapokuja, Na utukufu wake;
Tutafurahi milele, Kuka-a kwake Bwana.
1
Wewe umechoka sana? Wataka raha?
Kwake Yesu utapata - Msaada.
2
Alama anazo Yeye? Sana! Makovu
Ya mikono, na miguu, Na mbavu.
3
Naye amevikwa taji Kichwani Mwake?
Taji, kweli, alivikwa - Miiba!
4
Huku nikimfuata, Nipate nini?
Maonjo nje, na ndani - Amani.
5
Kwamba namwandama yeye, Mwisho ni nini?
Kurithi furaha naye - Milele.
1
Damu imebubujika, Ni ya Imanweli,
Wakioga wenye taka, Husafiwa kweli.
2
Ilimpa kushukuru Mwivi mautini;
Nami nisiye udhuru, Yanisafi ndani.
3
Kondo-o wa kuuawa, Damu ina nguvu,
Wako wote kuokoa Kwa utimilivu.
4
Bwana, tangu damu yako Kunisafi kale,
Nimeimba sifa zako, `taimba milele.
5
Bwana, umenikirimu Nisiyestahili
Kwa damu yako, sehemu Ya mali ya kweli.
6
Nikubali kukwimbia Mbinguni milele.
Mungu nitamsifia Jina lako pweke.
1
Yesu Mwokozi ili nitakaswe, nataka moyo uwe enzi yako.
Ukiangushe kilichoinuka unioshe sasa niwe mweupe.
Chorus
Mweupe tu, ndiyo mweupe,
Ukiniosha nitakuwa safi.
2
Bwana Yesu sasa unitazame, unifanye niwe dhabihu hai.
Najitoa kwako, na moyo, vyote; unioshe sana niwe mweupe.
3
Bwana kwa hiyo nakuomba sana, nakuongojea miguuni pako,
Wanaokuja hutupi kamwe, unioshe sasa niwe mweupe.
1
Naendea msalaba, Ni mnyonge, mpofu,
Yapitayo naacha nipe msalaba tu.
Chorus
Nakutumaini tu, ewe Mwana wa Mungu;
Nainamia kwako; niponye sasa, Bwana.
2
Nakulilia sana: nalemewa na dhambi;
Pole Yesu asema: "Nitazifuta zote."
3
Natoa vyote kwako, nafasi nazo nguvu,
Roho yangu na mwili viwe vyako milele.
4
Kwa damu yake sasa amenivuta sana,
Upendo hubidisha, nimtafute Mwokozi.
1
Bwana ninataka hili, kwa kuwa nimechafuka,
Kwa moto au kwa maji unisafishe kabisa.
Chorus
Unisafishe Mwokozi ndani, na nje, kwa moto
Utakavyo: ili dhambi ife kwangu, ife kwangu.
2
Kupewa hekima yote, itakuwa tunu kubwa;
Lakini moyo safi ni, bora kwangu, bora kwangu!
3
Mpaka moyo ni safi siwezi kuyafahamu
Mambo mazuri ya mbingu, mambo mazuri ya mbingu.
1
Wamwendea Yesu kwa kusafiwa. Kuoshwa kwa damu ya Kondoo?
Je, neema yake yatumwagiwa? Waoshwa kwa damu ya Kondoo?
Chorus
Kuoshwa kwa damu Itutakasayo ya Kondoo?
Ziwe safi nguo nyeupe sana; Waoshwa kwa damu ya Kondoo?
2
Wamwandama daima Mkombozi. Waoshwa kwa damu ya Kondoo?
Yako kwa Msulubiwa mavazi? Waoshwa kwa damu ya Kondoo?
3
Atakapokuja Bwana-arusi Uwe safi katika damu!
Yafae kwenda mbinguni mavazi: Yaoshwa kwa damu ya Kondoo?
4
Yatupwe yalipo na takataka; Uoshwe kwa damu ya Kondoo:
Huoni kijito chatiririka Uoshwe kwa damu ya Kondoo?
1
Nilipotoka kabisa, sasa narudi;
Nikakawia dhambini, Bwana narudi.
Chorus
Narudi nyumbani: daima kwako.
Kwa upendo nipokee: Naja nyumbani.
2
Nikasusurika sana, sasa narudi;
Mwenye uchungu natubu, Bwana narudi.
3
Nimechoka maovuni, sasa narudi;
Pendo lako lanivuta, Bwana narudi.
4
Ndilo tumaini langu, sasa narudi;
Yesu alinifilia, Bwana narudi.
5
Damu yake yanitosha, sasa narudi;
Unioshe kenyekenye, Bwana narudi.
1
Yesu anasema, "Wewe huna nguvu,
Kesha ukaombe, Na uje, Mwanagu."
Chorus
Alilipa bei, Nawiwa naye;
Dhambi ilitia waa, Aliiondoa.
2
Bwana, nimeona, Uwezo wako tu,
Waweza `takasa Mioyo michafu.
3
Sina kitu chema, kudai neema,
Hivi nitafua, Mavazi kwa damu.
4
Ninaposimama, Juu ya mawingu,
Taji nitaweka, Miguuni pa Yesu.
1
Msalaba wa Yesu, Nikae karibu;
Pale pana chemchemi Yakuponya dhambi.
Chorus
Pale msalaba Msalaba wake,
Huo ni sifa yangu Kwa maisha yote.
2
Karibu msalaba Nalitetemeka,
Pendo likaniona Likanirehemu.
3
Unikumbushe, Yesu. Nikuone pale:
Niupate upendo Na kuvutwa nao.
4
Karibu msalaba, Kwa kutegemea,
Kukesha na kungoja, Nitakaa pale.
1
Katika wenye dhambi,
Ndimi mkuu wao-
Ila Yesu ukaja,
Kwa dhambi alikufa,
Akamimina damu,
Niupate uzima.
2
Ajabu! Pendo lake!
Pendo lililo kuu,
Pendo lisilo mwisho,
Lidumulo milele-
Lililonitafuta
Ingawa sikumpenda
3
Ingawa ni mbaya
Kristo ni vyote kwangu;
Ajua haja zangu;
Huzuni zangu, zake;
Hata katika vita,
Akiwapo Salama.
1
Yote namtolea Yesu, moyo wangu ni wake:
Ninavutwa na upendo, kwa hivyo, najitoa.
Chorus
Yote kwa yesu, Yote kwa Yesu,
Upendo wako hushinda; Yesu, natoa.
2
Yote namtolea Yesu, Nainamia pake;
Nimeacha na anasa, kwako Yesu nipokee.
3
Yote namtolea Yesu, Nifanye niwe wako;
Nipe Roho yako, Bwana, anilinde daima.
4
Yote namtolea Yesu, nami naona sasa,
Furaha ya ukombozi, nasifu jina lake.
1
Yesu kwa imani, nakutumaini, peke yako
Nisikie sasa, na kunitakasa, ni wako kabisa
Tangu leo.
2
Nipe nguvu pia za kusaidia moyo wangu;
Ulikufa wewe, wokovu nipewe, nakupenda wewe,
Bwana wangu.
3
Hapa nazunguka katika mashaka, na matata;
Palipo na giza utaniongoza, hivi nitaweza,
Kufuata.
1
Umechoka, je, umesumbuka? Mwambie Yesu sumbuko lako;
Unayalilia yapitayo? Mwambie Yesu pekee.
Chorus
Mwambie Yesu, sumbuko lako, Yu rafiki amini,
Hakuna rafiki kama yeye, Mwambie Yesu pekee.
2
Je, machozi ya kulengalenga? Mwambie Yesu sumbuko lako;
Walemewa na dhambi rohoni? Mwambie Yesu pekee.
3
Waogopa shida na majonzi, Mwambie Yesu sumbuko lako;
Wasumbukia mambo yajayo? Mwambie Yesu pekee.
4
Kuwazia kifo kutisha? Mwambie Yesu sumbuko lako;
Watamania ufalme wake? Mwambie Yesu pekee.
1
"Uniangalie"atwambia, Yesu aliyetufia;
Msalabani ni uzima, Hapa utaipata hazina.
Chorus
Kutazama Kalwari, Kutazama Kalwari,
Ni kupewa kuishi Kuutazama mti wa Kalvari.
2
Ninapojaribiwa ghafula, Shetani hatanitega;
Nikitazama msalaba, Nguvu nitaipata kwa Bwana.
3
Msalaba nitautazama Kila wakati daima,
Ahadi nitategemea, Hivi kabisa sitaanguka.
1
Nina haja nawe kila saa;
Hawezi mwingine kunifaa.
Chorus
Yesu nakuhitaji vivyo kila saa!
Niwezeshe mwokozi, nakujia.
2
Nina haja nawe; Kaa nami,
Na maonjo haya, hayaumi.
3
Nina haja nawe; kila hali,
Maisha ni bure, uli mbali.
4
Nina haja nawe; Nifundishe,
Na ahadi zako, zifikishe.
5
Nina haja nawe; Mweza yote,
Ni wako kabisa, siku zote.
1
Nionapo amani kama shwari, au nionapo shida;
Kwa hali zote umenijulisha ni salama rohoni mwangu.
Chorus
Salama rohoni, Ni salama rohoni mwangu.
2
Ingawa shetani atanitesa, nitajipa moyo kwani,
Kristo ameona unyonge wangu; amekufa kwa roho yangu.
3
Dhambi zangu zote, wala si nusu, huwekwa msalabani;
Wala sichukui laana yake, ni salama rohoni mwangu.
4
Ee Bwana himiza siku ya kuja, panda itakapolia:
Utakaposhuka sitaogopa ni salama rohoni mwangu.
1
Namwandama Bwana kwa alilonena, Njia zangu huning`azia;
Na nikimridhisha atanidumisha, Taamini nitii pia.
Chorus
Kuamini, Njiani pweke ni hii
Ya furaha kwa Yesu: Amini ukatii.
2
Giza sina kwangu wala hata wingu,Yeye mara huviondoa;
Oga, wasiwasi, sononeko, basi; Huamini nitii pia.
3
Masumbuko yote, sikitiko lote; Kwa mapenzi hunilipia;
Baa, dhara, dhiki, vivyo hubariki. Taamini nitii pia.
4
Mimi sitajua raha sawasawa Ila yote Yesu kumtoa:
Napata fadhili na radhi kamili, Taamini nitii, pia.
5
Nitamfurahia na kumtumaini, Majumbani na njia-njia;
Agizo natenda; nikitumwa hwenda, Huamini, nitii pia.
1
Kumtengemea Mwokozi, kwangu tamu kabisa,
Kukubali neno lake, Nina raha moyoni.
Chorus
Yesu,Yesu namwamini, Nimemwona thabiti,
Yesu,Yesu, yu thamani, Ahadi zake kweli.
2
Kumtengemea Mwokozi, Kwangu tamu kabisa,
Kuamini damu yake, Nimeoshwa kamili.
3
Kumtengemea Mwokozi, Kwangu tamu kabisa,
Kwake daima napata, uzima na amani.
4
Nafurahi kwa sababu, Nimekutengemea;
Yesu,M-pendwa rafiki, uwe nami dawamu.
1
Yesu kwetu ni rafiki, hwambiwa haja pia:
Tukiomba kwa Babaye, maombi asikia:
Lakini twajikosesha,twajitweka vibaya:
Kama tulimwomba Mungu, dua alisikia.
2
Una dhiki na maonjo? Unamashaka pia?
Haifai kufa moyo, dua atasikia.
Hakuna mwingine Mwema, wa kutuhurumia:
Atujua tu dhaifu: maombi asikia.
3
Je, hunayo hata nguvu, huwezi kwendelea,
Ujapodharauliwa, ujaporushwa pia.
Watu wakikudharau, wapendao dunia,
Hukwambata mikononi, dua atasikia.
1
Kwa mahitaji ya kesho, Sina ombi;
Unilinde nisitende Dhambi leo;
Nisiseme neno baya, Mkombozi,
Nisifikiri uovu, Leo hivi.
2
Ningefanya kazi sawa Nakuomba;
Ningekuwa mtu mwema Kila saa;
Mapenzi yako nifanye, Na kutii;
Nitoe mwili dhabihu, Leo hivi.
3
Kama leo ningekufa Kwa ghafula,
Nitegemee ahadi Zako Bwana.
Kwa mahitaji ya kesho Sina ombi;
Uniongoze, nishike Leo hivi.
1
Bwana ni Mchunga, Sitahitaji;
Majani mabichi malisho yangu.
Ananinywesha maji matulivu;
Atanirudisha nikipotea.
2
Nipitapo bondeni mwa mauti
U mlinzi wangu sitaogopa;
Fimbo lako latosha kunilinda;
Ukinifariji sina hasara.
3
Kati ya mateso meza waandaa,
Na kikombe changu kinafurika;
Umenipaka kichwani mafuta;
Nitaulizaje zaidi kwako?
4
Wema na fadhili zinifuate
Siku zangu zote hata milele;
Nami nitakaa nyumbani mwa Bwana
Katika ufalme wa pendo lake.
1
Popote na Yesu nina furaha:
Anitumako Yesu ndiyo raha.
Asipokuwako hapanifai,
Akiwapo Yesu, mimi sitishwi.
Chorus
Popote, popote, sina mashaka;
Popote na Yesu naweza kwenda.
2
Akiwapo Yesu, si peke yangu;
Na nijapotupwa, akali wangu;
Ajaponiongoza njia mbaya,
Niwapo na Yesu nashukuria.
3
Akiwapo Yesu naweza lala,
Naweza pumzika hata kiyama;
Kisha nitakwenda kwake milele,
Akiwapo Yesu furaha tele.
1
Tafuta daima utakatifu;
Fanya urafiki na Wakristo tu;
Nena siku zote, na Bwana wako,
Baraka uombe kwa kila jambo.
2
Tafuta daima utakatifu;
Uwe peke yako ukimwabudu;
Ukimwangalia Mwokozi wako,
Utabadilishwa kama alivyo.
3
Tafuta daima utakatifu;
Kiongozi wako awe Yesu tu;
Katika furaha au huzuni,
Dumu kumfuata Yesu Mwokozi.
4
Tafuta daima utakatifu;
Umtawaze Roho moyoni mwako,
Akikuongoza katika haki,
Hufanywa tayari kwa kazi yake.
1
Saa heri ya maombi, sasa kwako tunarudi,
Sumbuku ya kuondoa, shida zetu na pungufu.
Taabuni mara nyingi, roho zetu zimepona,
Mashakani tumeshinda, wakati wa saa tamu.
2
Saa heri ya maombi, twapeleka dhiki zetu
Kwake aliyeahidi kubariki wenye haja.
Huagiza tumwendee, tutegemee neno lake,
Hivyo tumwekee yote, wakati wa saa tamu.
3
Saa heri ya maombi, tutazidi kuingia,
Bomani mwetu na ngome, hata tuishapo mwendo.
Yesu atatusikia, tutamtafuta daima,
Na tutakapokutana tutamwona - saa tamu.
1
Unifundishe, Baba; Ile njia ya sala;
Uniendeshe sana, Niwe kama Yesu.
Chorus
Niwe kama Yesu, Niwe kama Yesu,
Uniongoze, Baba; Niwe kama Yesu.
2
Unipe pendo, Baba, Watu kuwaokoa;
Nyumbani na mjini, Niwe kama Yesu.
3
Na unifahamishe, Wakati ndio mfupi;
Unibidishe, Bwana, Niwe kama Yesu.
1
Saa heri ya sala tunapojidhili,
Kama tukija kwake Yesu rafiki;
Tukiwa na imani kwamba yu mlinzi,
Waliochoka sana watapata raha.
Chorus
Saa ya sala, iliyo heri;
Waliochoka sana watapata raha.
2
Saa heri ya sala, ajapo Mwokozi,
Ili awasikie watoto wake.
Hutwambia tuweke miguuni pake
Mizigo yetu yote: tutapata raha.
3
Saa heri ya sala, wawezapo kuja Kwa Bwana
Yesu wanaojaribiwa;
Moyo wake mpole, atawarehemu;
Waliochoka sana watapata raha.
4
Saa heri ya sala tutakapopewa,
Mibaraka ya roho, tukimwamini;
Kwa kuamini kweli hatutaogopa;
Waliochoka sana watapata raha.
1
Nitakuandama kote, nitakapoagizwa
Wewe ukiniongoza nami nitaandama.
Chorus
Nitakuandama kote, naam, ulinifia;
Kwa neema yako Bwana napenda kuandama.
2
Njia ijapoparuza kwa miiba na fujo,
Ulitangulia mbele nami nitaandama.
3
Nijapokuta taabu na majaribu kote,
Nakumbuka shida yako, nami nitaandama.
4
Nijapoona ukiwa na mateso makali,
Wewe uliyatikiza nami nitaandama.
5
Ijapo wanipeleka vilindini mwa giza,
Wewe uliyatikiza nami nitaandama.
1
Uliniimbie tena, Neno la uzima;,
Uzuri wake nione, Neno la uzima;
Neno hili zuri, lafundisha kweli.
Chorus
Maneno ya uzima ni maneno mazuri
Maneno ya uzima ni maneno mazuri
2
Kristo anatupa sote, Neno la uzima:
Mwenye dhambi asikie, Neno la uzima:
Latolewa bure, Tupate wokovu:
3
Neno tamu la injili, Neno la uzima:
Lina amani kwa wote, Neno la uzima:
Litatutakasa, Kwa haki ya Mwana:
1
Nitwae hivi nilivyo, umemwaga damu yako,
Nawe ulivyoniita, Bwana Yesu, sasa naja.
2
Hivi nilivyo; si langu,kujiosha roho yangu;
Nisamehe dhambi zangu, Bwana Yesu, sasa naja.
3
Hivi nilivyo; sioni kamwe furaha moyoni,
Daima ni mashakani, Bwana Yesu, sasa naja.
4
Hivi nilivyo kipofu, maskini na mpungufu;
Wewe ndiwe u tajiri, Bwana Yesu, sasa naja.
5
Hivi nilivyo, mimi tu, Siwezi kujiokoa;
Na wewe hutanikataa, Bwana Yesu, sasa naja.
6
Hivi nilivyo; mapenzi yamenipa njia wazi;
Hali na mali sisazi, Bwana Yesu, sasa naja.
1
Chini ya msalaba Nataka simama;
Ndio mwamba safarini, Wa kivuli chema;
Ni kweli kwa roho yangu Ni tuo kamili,
Tatua mzigo wangu Wakati wa hari.
2
Hapa ni pema sana, Ni ngome kamili;
Hapa yameonekana, Mapenzi ya kweli;
Kama alivyoonyeshwa Yakobo zamani.
Msalaba umekuwa Ngazi ya mbinguni.
3
Na Yesu Msalabani Walimkemea,
Alikufa niokoke Niliyepotea:
Naona ajabu sana Ya mambo mawili
Jinsi alivyonipenda Nisiyestahili.
4
Atakayeonana Na Yesu mbinguni,
Njia yake aanzapo Ni Msalabani;
Wokovu upo hapa tu, Mwingine hapana.
Kisha kuna furaha kuu Pamoja na Bwana.
1
Nasikia mwito, Ni sauti yako;
Nikasafiwe kwa damu Ya kwangikwa kwako.
Chorus
Nimesongea mtini pako,
Unisafi kwa damu ya kwangikwa kwako.
2
Ni mnyonge kweli, umenipa nguvu;
Ulivyonisafi taka Ni utimilivu.
3
Yesu hunijuvya: Mapenzi imani,
Tumai, amani, rahi, hapa na mbinguni.
4
Napata wokovu, Wema na neema;
Kwako Bwana nina nguvu Na haki daima.
1
Baba sina msaada Ila kwako pekee:
Kama kwangu ungefichwa, Nifanyeje, Baba?
Chorus
Sasa hivi naamini Yesu alikufa,
Alimwaga damu yake, Nitoke dhambini.
2
Naamini mwana wako Nipe nguvu zako:
Nijazie mahitaji, Katika saa hii.
3
Ni furaha gani kwangu Kukuona uso!
Nijue sauti yako, Nipate neema.
1
Ni wako, Bwana, ninasikia Unaponena nami;
Lakini, kweli, nataka kwako Nizidi kusongea:
Chorus
Bwana vuta, (vuta) nije nisongee Sana kwako mtini.
Bwana, vuta, vuta, nije nisongee Pa damu ya thamani.
2
Niweke sasa nikatumike Kwa nguvu za neema;
Uyapendayo nami nipende Nizidi kukwandama.
3
Nina furaha tele kila saa Nizungumzapo nawe;
Ninanena kama kwa rafiki Nikipiga magoti.
1
Ulimwengu siutaki, Namtaka Bwana Yesu;
Dunia hunidanganya; Yesu yu mwaminifu.
Chorus
Rehema ni ya ajabu! Pendo bila kipimo!
Wokovu mkamilifu, Amana ya uzima!
2
Ulimwengu siutaki, Namtaka Bwana Yesu;
Kati ya dhoruba kali Yenye wimbo mtamu.
3
Ulimwengu siutaki, Namtaka Bwana Yesu;
Safarini duniani Yeye furaha yangu.
4
Ulimwengu siutaki, Namtaka Bwana Yesu;
Msalaba naamini, Hata namwona Yesu.
1
Twae wangu uzima, Sadaka ya daima;
Twae saa na usiku, Zikutukuze huku.
2
Twae mikono nayo, Ifanye upendavyo,
Twae yangu miguu, Kwa wongozi wako tu.
3
Twae sauti yangu, Niimbe kwa Mungu tu;
Itwae na midomo, Ijae neno lako.
4
Twae dhahabu pia, Na yote ya dunia;
Twae yangu hekima, Upendavyo tumia.
5
Nia itwae, Mungu, Haitakuwa yangu;
Twae moyo; ni wako, Uwe makazi yako.
6
Twae mapenzi yangu, Sifa za moyo wangu;
Twae kabisa nafsi, Niwe wako halisi.
1
Tawala ndani yangu, Ee Yesu, Mfalme.
Uwe kwangu majibu Kwa maswala yangu;
Uishi ndani yangu, Wewe, mwongozi
Utumishi ni wangu, Wako utukufu.
2
Hekalu nimetoa, Umelisafisha;
Sasa fahari yako Imulike ndani;
Dunia iwe kimya, Mwili sasa uwe
Mtumwa mtulivu Wa kukutii tu.
3
Viungo vyake mwili, Vyote vikungoja
Tayari vikiitwa Kwenda, kusimama;
Bila manung`uniko Au malaumu,
Au kusumbuliwa, Pasipo majuto.
4
Niwe na utulivu Pasipo haraka;
Tayari kungojea Maagizo yake.
Tawala ndani yangu. Ee Yesu, Mfalme,
Uwe kwangu majibu Kwa maswali yote.
1
Univute karibu, Baba, Unikumbatie;
Unisongeze kifuani, Nataka pumziko.
Chorus
Univute karibu (Vuta, univute karibu)
Kwa kamba za upendo, (Kwa kamba, kamba za upendo)
Univute (Kwa kamba za upendo, Univute karibu)
Karibu nawe. (Univute karibu)
2
Univute Mwokozi wangu, Na tusiachane;
Mikono yako juu yangu Leo niione.
3
Univute kwa Roho yako, Nifanane nawe;
Unioshe, unihuishe, Niwe safi, huru.
1
Kuwa wake Yesu, Je! Ni kusudi lako?
Ungeenda naye njia nyembamba?
Unataka aubebe mzigo wako?
Awe Mwongozi wako.
Chorus
Uwezo wake unakutosha
Na damu yake itakusafi;
Kwa vile ukubali ni bora
Afanye mapenzi yake nawe.
2
Unataka kuitika anapokwita?
Kupata amani kwa kumpa vyote?
Wataka uwezo usianguke kamwe?
Awe Mwongozi wako.
3
Wataka raha katika ufalme wake?
Ungeshinda kwa majaribu yote?
Ungefanya kazi yake vizuri sana?
Awe Mwongozi wako.
1
Hacha, maneno mabaya Yasitoke Kinywani
Moyo mwema uzuie Ndimi, zisichafuke
Chorus
"Nanyi pendeni", Asema Yesu, (mpendane) (mpendane)
Kama mwanzo alivyotupenda:
"Nanyi pendeni", Asema Yesu, (mpendane) (mpendane)
Wana, tiini amri hii. (amri heri hii).
2
Pendo ni mtakatifu; Urafiki: mzuri:
Visiharibike mara Kwa kunena vibaya.
3
Tusinene kwa hasira, Inazaa huzuni.
Pendo lako, ee Mwokozi, Inatosha tushinde.
1
Huniongoza Mwokozi, ndipo nami hufurahi,
Niendapo pote napo, ataniongoza papo.
Chorus
Kuongoza hunishika; kwa mkono wa hakika;
Nitaandamana naye Kristo aniongozaye.
2
Pengine ni mashakani nami pengine rahani;
Ni radhi, ijayo yote, yupo nami siku zote.
3
Mkono akinishika kamwe sitanung`unika;
Atakachoniletea ni tayari kupokea.
4
Nikiisha kazi chini sitakimbia mauti;
Kushinda ni ya hakika nikiongozwa na Baba.
1
Karibu na wewe, Mungu wangu; Karibu zaidi, Bwana Wangu.
Siku zote niwe karibu na wewe, Karibu zaidi, Mungu wangu.
2
Mimi nasafiri duniani, Pa kupumzika sipaoni,
Nilalapo niwe karibu na wewe, Karibu zaidi, Mungu wangu.
3
Yote unipayo yanivuta; Pa kukaribia nitapata;
Na nielekezwe karibu na wewe; Karibu zaidi, Mungu wangu.
4
Na kwa nguvu zangu nikusifu, Mwamba, uwe maji ya wokovu;
Mashakani niwe, karibu na wewe, Karibu zaid, Mungu wangu.
5
Na nyumbani mwa juu, Baba yangu; Nikinyakuliwa toka huko,
Kwa furaha niwe pamoja na wewe, Karibu zaidi Mungu wangu.
1
Fikira moja tu Hurejea tena;
Nimekaribia mbingu Zaidi ya jana.
Chorus
Karibu na kwetu mbingu,
Karibu na kwetu sasa, Nikwone karibu.
2
Karibu na kwetu Na kwenye makao;
Kiti cha enzi cha Mungu, Pahali pa mto.
3
Kamilisha, Yesu, Kuamini kwangu;
Nikifika mwisho wangu, Nikwone karibu.
1
Yanipasa kuwa naye, Mwokozi Bwana wangu.
Akiwa karibu nami, napata nguvu kweli.
Chorus
Moyo hauogopi, wala kutikisika.
Nitakwenda apendapo, kwa kuwa anilinda.
2
Yanipasa kuwa naye, kwani nategemea;
Anaweza kufariji na maneno matamu.
3
Yanipasa kuwa naye maisha yangu yote;
Yakiwapo majaribu na mashaka yo yote.
4
Yanipasa kuwa naye katika njia zangu;
Macho yake yaongoza hatua zangu zote.
1
Njiani huniongoza Yesu wangu, Mwokozi:
Rehema hatapunguza, Milele Kiongozi.
Ina raha kwandamana Duniani daima:
Nijaposumbuka sana, yeye hutenda vyema.
2
Njiani huniongoza Hupunguza matata;
Nikiungua hupoza. Na njaani nashiba.
Lichokapo guu langu Nguvu zikapungua.
Jiwe lilo mbele yangu hunibubujika.
3
Njiani huniongoza Kwa pendo zilizo kuu,
Mwisho atanituliza Kwake Baba yangu juu,
Nikivikwa kutokufa, Nikae na Mwokozi,
Nitamsifu sana; sifa: " Kweli ni Kiongozi."
1
Uniongoze, Yehova, Ni msafiri chini;
Ni mnyonge, u hodari, `Nilinde kwa mkono.
Unitunze, unilinde, Unionyeshe njia!
2
Na kisima cha uzima, Maji ya utabibu,
Fungua kwa moyo wangu, Ninywe na kuponyeka!
Uninyweshe, unilishe, Hata nimetosheka.
3
Wakati wa kuuvuta, Ule mto Yordani,
Hofu yangu ufariji, `Nione uso wako.
Nyimbo shangwe, nyimbo shangwe, Nitaimba daima.
1
Mfalme yu mlangoni, Ndiye aliyetufia;
Mara wote wampendao atawakusanya.
Chorus
Yuaja, yuaja, mlangoni anasimama;
Anakuja, anakuja, Kuja kwake karibu.
2
Dalili za kuja kwake Zinazidi kutimizwa;
Karibu wateule watamlaki Bwana.
3
`Sitafute duniani amani wala furaha,
Mpaka Bwana arudi dhambi kuondoa.
4
Tutakaa na Mwokozi Makaoni ya milele;
Daima tutafurahi kuwa watu wake.
1
U mwendo gain nyumbani? Mlinzi akanijibu,
"Usiku sasa waisha, macheo karibu."
Usihuzunike tena, bali ulemee mwendo
Hata ushike ufalme kule mwangani juu.
2
Na tena niliuliza, nchi yote ikajibu;
"Sasa mwendo watimika, milele karibu."
Usihuzunike tena, ishara kuu zasonga
Na viumbe vyangojea sauti ya Bwana.
3
Nikamwuliza shujaa, ndivyo kanitia moyo:
"Shikilia mapigano, kitambo yaisha."
Usihuzunike tena, kazi ifanywe kwa moyo;
Tumeahidiwa tunu tuishapo shinda.
4
Siyo mbali na nyumbani! Fikira tamu njiani,
Latupoza roho, nalo lafuta machozi.
Usihuzunike tena, kitambo tutakutana
Wenye furaha kamili nyumbani mwa Baba
1
Anakuja upesi, Yesu Bwana wetu,
Msafiri mbali na kwao;
Alisema dhahiri, "Nitakuja tena";
Amina; na uje, E Bwana.
Chorus
Yuaja, Yesu atarudi sasa;
Anakuja duniani.
Wasafiri wote watapumzika,
Yesu anaporudi tena.
2
Makaburi yote wafu wanapolala,
Yatafunguliwa tena;
Na mamilioni pale wataondoka tena,
Wasione machozi kamwe.
3
Hatutatengana na hao tena huko;
Nyimbo nzuri tutaimba.
Watakusanyika `toka kila kabila,
Miguuni pa Mwana-Kondoo.
4
Aleluya Amin! Aleluya tena!
Upendo wake unashinda!
Tutamsifu milele, hata tutashangaa,
Jinsi alivyotukomboa.
1
Watakatifu kesheni, nguvu za mbingu zagonga;
Washeni taa tayari kwa kurudi kwake Bwana.
Chorus
Yuaja, Yesu Mfalme, Yuaja mwenye fahari,
Yesu yuaja enzini Karibu Yesu, uje.
2
Piga mbiu, tangazeni habari ya ukombozi.
Ya Mponya wa upendo nayo nguvu ya samaha.
3
Falme nyingi zaangushwa, Panda ya saba hulia;
Tanga neema yake kabla ya kupita saa.
4
Mataifa yapotea, nchi zajaa uchungu:
Kristo anaharakisha, Unabii unatimizwa.
5
Wenye dhambi njoni sasa Kristo awapatanishe,
Mbio twaeni neema, kitambo muda waisha.
1
Piga panda na ya makelele; Yesu yuaja tena!
Ipaze sauti, imba sana; Yesu yuaja tena!
Chorus
Anakuja, anakuja; Yesu yuaja tena!
2
Itoe mwangwi sana vilima; Yesu yuaja tena!
Yuaja kwa utukufu mwingi, Yesu yuaja tena!
3
Itangaze mahali po pote, Yesu yuaja tena!
Mwokozi aliyetufilia, Yesu yuaja tena!
4
Kuona machafuko twajua Yesu yuaja tena!
Mataifa yakasiriana, Yesu yuaja tena!
5
Maradhi, hofu hutuhubiri Yesu yuaja tena!
Taabu, njaa hutulilia Yesu yuaja tena!
1
Tumaini liko La thamani kuu,
Kupita anasa tupu zake ulimwengu.
2
Pana nyota nzuri: Nuru itoayo,
Kwetu wakati wa kifo Ndio ufufuo.
3
Zikiumwa roho Na hofu, mashaka,
Sauti hutuambia Mungu hutupenda.
4
Kutoka Kalwari Sauti hunena;
Nyota ni nuru ya mbingu, Tumaini letu.
1
Pengine ni saa ya kupambazuka,
Mishale ya jua ipenyapo giza,
Kwamba atakuja Yesu mtukufu,
Awapokee wake.
Bwana itakuwa lini Tutapoimba,
"Anakuja, Bwana Yesu, Aleluya,
Amin, Aleluya, Amin?"
2
Pengine mchana, pengine jioni,
Pengine usiku wa manane, giza,
Itatoweka kwa fahari akija,
Awapokee wake.
3
Majeshi yake yataimba "Hosana,"
Na watakatifu waliotukuzwa,
Watamsifu kwa kuwa amekuja,
Awapokee wake.
4
Furaha tukiitwa pasipo kufa,
Pasipo kuona maradhi, machozi;
Kuchukuliwa winguni kwa fahari,
Akija kwa watu wake.
1
Unakaribia wakati wa Kuja kwa Yesu.
Atawachukua watu wake Nyumbani juu.
Chorus
Tunaiona mishale ya nuru Inayopenya giza;
Tunaiona mishale ya nuru Ya ufunuo.
2
Injili inatangazwa pote kwa mataifa;
Bwana wa Arusi atakuja Na tarumbeta.
3
Pamoja na malaika zake Bwana arudi,
Awapeleke waaminifu Wasife tena.
4
Wapenzi waliotengwa kale Watakutana;
Machozi yao wenye huzuni Yatafutika.
1
Ahadi tamu kwa waamini,
Tazama nakuja upesi sana.
Uwe imara, hatari kubwa:
Ndugu usilale, bali ukeshe.
Chorus
Uihifadhi imani yako,
Dunia mpya itatolewa
Njoo ingia furaha yangu;
Taji zinangoja; Uwe imara.
2
Tatakesha na kutoa sala;
Atakuja kama mwivi kwa wengi;
Ya kwamba yu karibu twajua,
Ila hatujui ni siku gani.
3
Tunategemea Neno lake,
Ambalo latangaza kuja kwake,
Tumaini letu ni ahadi:
"Naja karibuni, uwe imara."
1
Furaha kwa ulimwengu, Bwana atakuja!
Kila moyo umpokee, Viumbe imbeni,
Viumbe imbeni, Viumbe vyote imbeni.
2
Na Bwana atatawala: Watu na waimbe;
Mit, milima na mawe Kariri furaha,
Kariri furaha, Kariri furaha kubwa.
3
Atatawala kwa wema; Atawafundisha
Mataifa haki yake, Ajabu za pendo,
Ajabu za pendo, Ajabu za pendo lake.
1
Yesu Bwana Mwokozi aishi milele,
Najua kwamba Yupo pamoja na mimi;
Sauti nasikia, Rehema naona;
Wakati namhitaji, yupo nami.
Chorus
Yu hai, Yu hai,Yu hai Bwana Yesu!
Atembea, azungumza nami siku zote.
Yu hai, Yu hai, kutoa uzima!
Hivi ndivyo nijuavyo,
Yu hai ndani yangu!
2
Ulinzi Wake upo naona dhahiri,
Miguu ichokapo, sikati tamaa;
Najua an`ongoza kupota dhoruba,
Siku ya kuja kwake nitamwona.
1
Tarumbeta ya mwana itakapolia mara,
Milele itakapopambazuka,
Nao wa haki watakapokusanyika ng`ambo,
Majina yaitwapo, lo!
Chorus
Majina yaitwapo, lo! -
Majina yaitwapo, lo! -
Majina yaitwapo, lo! -
Majina yaitwapo, lo! -
Niweko.
2
Siku ile watakatifu watakapoamka,
Na kuondoka huru kaburini;
Watakapokusanyika makaoni kule juu,
Majina yaitwapo, lo!
3
Tutende kazi kwa yesu mchana kutwa kwa bidii,
Tutangaze kote pendo lake kuu;
Nayo kazi itakapotimika hap chini,
Majina yaitwapo, lo!
1
Hapo Yesu atakapoita mataifa mbele yake,
Tutashindaje kwenye hukumu mbele ya kiti cha enzi?
Chorus
Atakusanya ngano ghalani, atatupambali makapo;
Tutashindaje hukumuni siku kuu ya kiyama?
2
Je, tutasikua neno tamu: "vema, wewe mtumwa mwema,"
Ama wenye uchunguna hofu tutakatazwa ufalme?
3
Atakubali tu kwa furaha watoto wake wapendwa,
Atawapa mavazi meupe, wakea tayari kumlaki.
4
Hivyo tukeshe, nasi tungoje, wenye taa zinazo waka;
Tutakapoitwa arusini tuwe tayari kumlaki.
5
Roho ikielekea mbingu twangoja wenye saburi,
Hata safari yetu iishe, tukae kwake milele.
1
Sitafuti mali, wala utajiri; Nataka kwa yakini nipate Mwokozi.
Chuoni mwa Ufalme, niambie Yesu, Jina langu yakini limeandikwa, je?
Chorus
Limeandikwa, je? Jina langu huko?
Kitabuni mbinguni, limeandikwa, je?
2
Dhambi zangu ni nyingi, ni kama mchanga, Lakini damu yako, Mwokozi, yatosha;
Kwani umeahidi: zijapo nyekundu Zitakuwa nyeupe ilivyo theluji.
3
Mji mzuri sana, wa majumba makuu, Walipo malaika, mji bila ovu;
Wakaapo walio na mavazi safi, Limeandikwa sasa, jina langu huko?
1
Imeanzishwa hukumu mbinguni; tutasimamaje pale;
Apimapo Mungu Hakimu kila wazo na tendo?
Chorus
Tutasimamaje sote katika siku kuu ile?
Dhambi zetu zitafutika ama zitatuangusha?
2
Wametangulia wafu kupimwa, Kitambo ndipo wahai;
Watapokea neno la mwisho, Vitabuni mwa Mungu.
3
Tutasimamaje usiku ule, Siri zetu, kila moja,
Zafunuliwa toka vitabu; Yesu atusaidie!
1
Mfalme wetu atuita tukae karamuni kwake;
Itakuwaje nasi kule Bwana ajapo?
Chorus
Bwana ajapo, ndugu, Bwana ajapo!
Itakuwaje na sisi, Bwana akija?
2
Atavikwa vizuri sana, taji badala ya miiba;
Kweli tokeo la fahari Bwana ajapo.
3
Kwa furaha awakubali wenye mavazi ya arusi;
Tu wa heri tukimridhisha Bwana ajapo.
4
Kutakuwako na utengo: watalia waliomwasi;
Cha kutisha kitambo kile Kristo ajapo!
5
Mfalme utupe neema sisi tunapokungoja,
Tusiogope kukuona ujapo Bwana.
1
Hatujui sa-a ya kuja kwa Bwana,
Lakini dalili zasema karibu,
Atakaporudi, -lakini kwa kweli,
Hatujui sa-a.
Chorus
Atakuja, kwa vile tukeshe;
Atakuja Mwokozi, Aleluya!
Atakuja kwa fahari ya Baba yake,
-Hatujui saa.
2
Pana nuru kwao wapendao haki,
Pana kweli katika Chuo Cha Mungu;
Unabii hufundisha kuja kwake,
-Hatujui saa.
3
Tutakesha tutaomba daima,
Tutafanya kazi mpaka akija;
Tutaimba na tutasoma ishara,
-Hatujui saa.
1
Sijui atakapokuja, Mchana au usiku;
Labda sa-a ya alasiri. Pengine ni alfajiri.
Hutwambia tuwe tayari, Ta-a zetu tusizime;
Ili ajapo atukute; Tuwe tukimngoja Yeye.
Chorus
Tukimngojea, (Kukesha, tunakungoja Wewe)
Tukimngojaa, (Kukesha, tunakungoja Wewe)
Tukimngojaa, (Kukesha, tunakungoja Wewe)
Twakesha, twamngoja Yeye.
2
Nakumbuka huruma zake, Bei ya wokovu wetu;
Aliacha nyumba tukufu Awafilie wabaya.
Ninadhani itampendeza, Kama sisi watu wake,
Tukionyesha pendo letu, Tuwe tukimngoja Yeye.
3
Ee Yesu, Mwokozi mpendwa, Wajua nalihifadhi
Tumaini la kukuona. La kukaribishwa nawe.
Ukija kwa watu wengine, Kama mhukumu wao,
Kwangu utakuwa rafiki, Nakesha, nakungojea.
1
Nitaonana na Yesu, uso kwa uso kweli;
Siku ile shangwe tele nikimwona Mwokozi
Chorus
Tutaonana kwa macho, huko kwetu mbinguni;
Na kwa utukufu wake nitamwona milele.
2
Sasa siwezi kujua jinsi alivyo hasa,
Bali atakapokuja, nitamwona halisi.
3
Mbele yake yafukuzwa machozi na huzuni;
Kipotovu kitanyoshwa, fumbo litafumbuka.
4
Uso kwa uso! Hakika palepale furaha;
Nitafurahi kabisa nikimwona Mwokozi.
1
Ati tuonane mtoni? Maji mazuri ya mbingu;
Yanatokea mwangani, penye kiti cha Mungu.
Chorus
Naam, tuonane mtoni! Watakatifu, kwenu ni mtoni!
Tutakutanika kule mtoni penye kiti cha Mungu.
2
Tukitembea mtoni na Yesu Mchunga wetu,
Daima tu ibadani usoni pake kwetu.
3
Tukisafiri mtoni tutue ulemeao
Wema wa Mungu yakini; una taji na yao!
4
Kwang`ara sana mtoni cha Mwokozi ni kioo,
Milele hatuachani tumsifu kwa nyimbo.
5
Karibu sana mtoni, karibu tutawasili,
Mara huwa furahani na amani ya kweli.
1
Kazi yangu ikisha,nami nikiokoka;
Na kuvaa kutokuharibika,
Nitamjua mwokozi nifikapo ng`amboni;
Atakuwa wa kwanza kunilaki.
Chorus
Nitamjua,Nitamjua,nikimwona uso kwa uso;
Nitamjua,Nitamjua,kwa alama za misumari.
2
Furaha nitapata nikiona makao`
Bwana aliyotuandalia;
Nitamsifu Mwokozi kwa rehama na pendo;
Vilivyonipa pahali mbinguni.
3
Nao waliokufa katika Bwana Yesu,
Nitawaona tena huko juu;
Lakini nifikapo kwake huko mbinguni,
Nataka kumwona Mwokozi kwanza.
4
Milangoni mwa mji Bwana atanipisha,
Pasipo machozi wala huzuni.
Nitauimba wimbo wa milele;lakini
Nataka kumwona mwokozi kwanza.
1
Ukingoni mwa Yordani ninaangalia
Bara nzuri ya Kanaani, ninayotamani.
Chorus
Tutakaa pamoja na Yesu, Katika pwani yenye raha;
Tutaimba wimbo wa Musa na Kondoo, Milele hata milele.
2
Bara ile ina nuru, nuru ya milele;
Kristo, Jua, hutawala, hufukuza giza.
3
Nitapafikia lini na kubarikiwa,
Penye ufalme wa Baba, na kumwona uso?
4
Furaha yangu rohoni ni kuchukuliwa;
Siyaogopi mawimbi katika Yordani.
1
Wavunaji watafurahi, pale watakaporudi,
Wakiyaleta mavuno hata Yerusalemu.
Chorus
Furaha wataipata, furaha hata milele,
Furaha, wataipata, wakati wa mavuno.
2
Na siku ile tutaimba, kumshukuru na kumsifu,
Bwana Yesu Jumbe wetu, kule Yerusalemu.
3
Wavunaji watafurahi makaoni mwa milele,
Yaliyowekwa tayari kule Yerusalemi.
1
Pana mahali pazuri mno, Twapaona kwa mbali sasa;
Baba yetu angoja pale, Amepanga makao yetu.
Chorus
Kitambo tu bado, Tutakutana ng`ambo pale.
Kitambo tu bado, Tutakutana ng`ambo pale.
2
Tutaimba pale kwa moyo Nyimbo tamu za wenye heri.
Na rohoni hatutaona Tena haja ya kupumzika.
3
Kwa baba yetu mkarimu Tutatoa shukrani sana.
Kwa kipaji cha pendo lake Na baraka anazotupa.
1
Mahali pa maji mazuri maji ya uzima;
Anapotungoja Yesu tutakaribishwa.
Chorus
Mahali pa maji mazuri, penye maji ya uzima;
Tutakaa na Mwokozi, chemchemi ya uzima.
2
Tunapochoka safarini, tamu kupumzika.
Panapo maji ya uzima yatufurahisha.
3
Una kiu? Uje kwa Yesu, utaburudishwa;
Yesu yu maji ya uzima, unywe,uokoke.
1
Mchana hauishi Mjini mzuri;
Mji hautapita; Na hapana giza.
Chorus
Machozi yatafutwa, Kifo hapana pale;
Hawahesabu siku, Na hapana giza.
2
Milango ni ya lulu, Mjini mzuri;
Dhahabu njia zake; Na hapana giza.
3
Milango haifungwi Mjini mzuri;
Mto ni wa uzima Na hapana giza.
4
Hawahitaji jua Mjini mzuri,
Mwana Kondoo nuru; Na hapana giza.
1
Furaha na raha tutapata, Furaha na raha tutapata,
Furaha na raha tutapata Yesu anaporudi.
Chorus
Yesu anaporudi (rudi) Yesu anaporudi (rudi);
Furaha na raha tutapata Yesu anaporudi.
2
Tutaimba nyimbo za shangwe kuu, Tutaimba nyimbo za shangwe kuu,
Tutaimba nyimbo za shangwe kuu Yesu anaporudi.
3
Hapana machozi arudipo, Hapana machozi arudipo,
Hapana machozi arudipo, kwa wateule wake.
1
Vitu vyote ni sawa, panapo pendo:
Kila sauti tamu, panapo pendo
Pana amani pale, na furaha nyumbani,
Siku zote salama panapo pendo.
Chorus
Panapo upendo
Panapo pendo.
2
Furaha I nyumbani, panapo pendo:
Hapana machukizo, panapo pendo;
Chakula ni kitamu, mashamba yasitawi,
Maisha ni kamili, panapo pendo.
3
Hata mbinguni juu, pana furaha
Wakiona upendo nyumbani mwetu.
Macho yapendezwa na viumbe vya Mungu,
Naye Mungu huona, panapo pendo.
4
Ee Yesu niwe wako, wako kabisa,
Ndipo patakuwako Pendo nyumbani;
Nitakaa salama, sitafanya dhambi:
Nitabarikiwa tu panapo pendo.
1
Mungu u mapenzi mtakatifu Yapitayo fahamu za watu
Twanyenyekea sisi wapungufu, Wape baraka wapenzi wetu.
2
Ewe Mapenzi yasiyopimika Twawaombea kitini Mwako,
Wape mapenzi yasiyotindika, Waliooana mbele yako.
3
Ewe uhai, wewe u dhamana Ya imani na matumaini,
Wape kuvumilia hapa sana Wasiche maumivu mwishoni.
4
Wape furaha hiyo iwezayo kutia nuru kwenye huzuni,
Wape amani hiyo itakwayo Katika matata duniani.
5
Waende mbele kusaidiana Maisha yao ulimwenguni;
Hata mwisho, ni kuja kwake Yesu, Wafurahi milele mbinguni.
1
Tuonanapo na rafiki sote twafurahi,
Ila tumepaswa mwishowe kuagana tena.
Chorus
Hatutaagana tena nyumbani mbinguni,
Kwenye nchi tamu juu, Hatutaagana.
2
Twatumaini kwa furaha tutaonana juu
Na rafiki tulioaga tuishapo shinda.
3
Kule hatutatamka kamwe neno la kuaga,
Tutaimba daima tena nyimbo za furaha.
1
Kufariki naye Yesu! Usingizi wewe heri;
Raha isiyofujika kwa majozi na adui.
2
Kufariki naye Yesu! Lo! Ya kubwaga simanzi
Na kulala na amani hata Bwana awatuze.
3
Kufariki naye Yesu! Heri watakaoamshwa,
Wataona siku ile utukufu wake Bwana.
4
Kufariki naye Yesu! Wataamka aitapo;
Watapasua kaburi na kutoka watukufu.
1
Wimbi la damu ya Yesu Linatutakasa;
Aliumia kusudi Tupate uzima.
Chorus
Wimbi la damu naona, Naingia, natakaswa!
Bwana asifiwe sana, Hutakasa, hutakasa.
2
Damu inasema kwangu, Nasikia mvuto;
Inasema, moyo wangu Hutakaswa nayo.
3
Naondoka kutembea Kwa nuru ya mbingu;
Mavazi yamesafishwa; Moyoni ni Yesu.
4
Neema ni ya ajabu, Kutakaswa ndani!
Na kuwa naye Yesu tu, Aliye Mwokozi.
1
Mimina upya nguvu toka juu;
Tupe pendo lako, ewe Mwokozi.
Chorus
Twakusihi sana Yesu Mwokozi,
Tubatize upya, kwa Roho leo.
2
Kwako twalia, wenye maovu,
Osha moyo wetu, ututakase.
3
Kipaji cha juu, kitume kwetu,
Tubariki sasa, utufariji.
4
Isikilize, kwa moyo wazi,
Sauti ya Roho; ubarikiwe.
1
Raha yangu yote, Bwana, I mbavuni pako;
Mimi sina haja tena ila kifo chako.
2
Mwokozi uliyekufa, nawe ndiwe Mungu,
Kifo chako ni kwa dhambi, ziondoe zangu.
3
Nioshe na niwe wako, nawe uwe wangu;
Nioshe damuni mwako liwe fungu langu.
4
Nioshe si miguu tu, osha tangu nyayo,
Hata kichwa changu juu, na ndani ya moyo,
5
Na iwe kafara damu nifanyapo kazi,
Hata imani itimu, nikwone,Mwokozi.
1
Mkate wa mbingu mega kwetu;
Ulivyotoa kwa thenashara.
Katika kitabu, twakuona.
Moyo unatweta kukutana.
2
Neno la ukweli libariki;
Tusikie mwito wa upole.
Vizuizi vyote vitakoma.
Tena tutapata uungwana.
3
Uzima na nguvu, utanena;
Nakimbiliza tu kufuata.
Lakini mnyonge ndiye mimi;
Naye Mshindaji ndiye wewe!
1
Mwamba wenye imara,kwako nitajificha!
Maji hayo na damu yaliyotoka humu,
Hunisafi na dhambi,Hunifanya m-shindi.
2
Kwa kazi zote pia sitimizi sheria,
Nijapofanya bidii,nikilia na kudhii,
Hayaishi makosa;ndiwe wa kuokoa.
3
Sina cha mkononi,naja msalambani,
Nili tupu,nivike;ni mnyonge,nishike;
Nili mchafu,naja,nioshe nisijafa.
4
Nikungojapo chini,na kwenda kaburini,
Nipaapo mbinguni na kukwona enzini,
Roho yangu na iwe rahani mwako wewe
1
Sauti ya Mchungaji, ninasikia jangwani,
Kondoo waliopotea anwaita warudi.
Chorus
Leteni, leteni, leteni toka dhambini;
Leteni, leteni, waleteni kwa Yesu.
2
Nani atakeyekwenda amsaidie Mchungaji,
Awarudishe zizini, wasife bure gizani?
3
Usikose kusikis sauti ya Mchungaji,
"Kondoo waliopotea nwnda na kuwatafuta."
1
Twaomba, Bwana, umpokee Kama mhudumu;
Ambaye anjitoa Kuwa mtumishi.
2
Twaomba, Bwana, umpokee Kama mhudumu;
Neno lako alitoe, Mwangaza kung`aa.
3
Mwokozi wetu, twaomba, na umwandikie
Kitabuni mwako juu Mjumbe wa injili.
4
Silaha zake apewe Kumshinda adui;
Vitabuni awe hohari, Mpaka mauti.
5
Yeye ashindaye, Bwana, Kwa rehema yako,
Ile taji ya dhahabu, Nawe utampa
1
Msingi wa Kanisa Ndiye Yesu Bwana;
Kiumbe chake kipya Akipenda sana;
Kutaka ‘kitafuta Alishuka chini,
Naye kwa haja yake, Akafa Mtini.
2
Lina kila kabila Kisha ndiyo moja
Wokovu wake una Mwokozi ndiyo moja;
Uzazi ni umoja. Moja tumaini.
Chakula ni kimoja. Moja tumaini.
3
Watu hustaajabu Kwa mashaka yote.
Yaipatayo nje Hata ndani mwote;
Ila watakatifu Humwomba, wakikesha
Usiku ni kilio. Asubuhi raha.
4
Mashaka na taabu Hata vita vyake.
Vyangoja matimizo Ya amani yake.
Ndipo kwa macho yetu Twone utukufu
Kanisa ya kushinda itastarehe juu.
1
Kitambo Bwana yuaja, atafute kote
Vito vya thamani kubwa: mali yake kuu.
Chorus
Kama nyota tajini vitang`aa sana,
Vito vizuri kweli vyenye thamani.
2
Karibu atakusanya vito kwa ufalme,
Vizuri vinavyong`aa: mali yake kuu.
3
Watoto wote wadogo wampendao Yesu,
Ndiyo vito ving,vyo: mali yake kuu.
1
Anipenda ni kweli: Mungu anena hili;
Sisi wake watoto kutulinda si zito.
Chorus
Yesu Mwokozi ananipenda;
Kweli hupenda, Mungu amesema.
2
Kwa kupenda akafa niokoke na kufa:
Atazisafi taka sana ataniweka.
3
Anipenda kabisa; niuguapo sasa,
Anitunza mbinguni niliyelala chini.
4
Kunipenda haachi tu sote hapa chini,
Baada ya mashaka kwake tanipeleka
1
Nilinawa mikono safi asubuhi,
Itende kazi kutwa kwa Yesu, Yesu Mwokozi.
Chorus
Kaza sana macho njiani kote,
Utende kwa Yesu kazi njema tu.
2
Natega masikio nitambue wasaa,
Mikono na itende upole daima.
3
Macho yangu yachunga mikono kazini;
Ilindwe maovuni impendeze Yesu.
1
Upendo ni furaha, ni kweli desturi;
Yake kuzisahihisha, njia zetu zote.
Chorus
Yu pendo: tu watoto wake,
Yu pendo, Mwana wa Mungu!
2
Na sisi tupendane kama Baba Mungu,
Amri yake ndiyo hii, kupendana sana.
3
Duniani huzuni, ugonjwa mauti;
Kwa pendo tuwafariji, wenye mahitaji.
4
Na atakapokuja kutuchukua juu;
Tutaimba milele pendo lake Yesu.
1
Baba yetu aliye mbinguni,
Amenifurahisha yakini.
Kuniaambia mwake Chuoni,
Ya kuwa name Yesu pendoni.
Chorus
Anipenda Mwokozi Yesu,
Anipenda, Anipenda;
Anipenda Mwokozi Yesu,
Anipenda mimi.
2
Nimuachapo kutanga mbali,
Yeye yu vivyo, hupenda kweli:
Hunirejea kwake moyoni,
Kweli yu name Yesu pendoni.
3
Anipenda! Nami ninampenda,
Kwa wokovu alionitenda;
Alinifilia msalabani,
Kwa kuwa name Yesu pendoni.
1
Mungu huona videge wanaoanguka;
Akiwapenda videge, vile hunipenda.
Chorus
Hunipenda, hunipenda, hunipenda pia;
Najua ananipenda niliye mdogo.
2
Rangi ya namna nzuri hupamba maua;
Akiyapenda maua, vile hunipenda.
3
Mungu aliyeviumba videge, maua,
Hatasahau watoto, kweli huwapenda.
1
Sikia mlio! Pesa koponi
Zinalialia
Chorus
Kuanguka kuanguka pesa koponi,
Kila moja kwako, Yesu zipokee.
2
Huanguka pesa toka mikono:
Sadaka kwa Yesu ya kundi dogo.
3
Tulio wadogo tuna haba tu;
Tuishapo kua pendo `tazidi.
4
Wenye mali chache tumpe moyo;
Kwa furaha tupu atakubali
1
Siku sita fanya kazi, Ya saba ni kwa Yesu.
Hapo tunapopumzika, kwani ni yake Yesu.
Chorus
Moja, mbili, tatu, nne, tano, sita, zote kwetu;
Lakini tutakumbuka, Ya saba ni kwa Yesu!
2
Huonyesha ya kufanya, Kwa kuwa ni ya Yesu,
Na atuonyesha njia, tutamfuata Yesu.
3
Tuombe kila Sabato, Na kujifunza kwake;
Tutamtii daima, tutakaa na Yesu
1
Kuwa na Yesu nyumbani, Furaha nyingi,
Furaha nyingi, furaha nyingi.
Kuwa na Yesu nyumbani.
Furaha nyingi, furaha nyingi.
2
Yesu yu ndani ya Baba, Nyumba salama,
Nyumba salama, nyumba salama;
Yesu yu ndani ya Baba.
Nyumba salama, nyumba salama.
3
Yesu yu ndani ya Mama, Nyumba salama,
Nyumba salama, nyumba salama;
Yesu yu ndani ya Mama.
Nyumba salama, nyumba salama
4
Yesu ndani ya watoto, Nyumba salama,
Nyumba salama, nyumba salama;
Yesu yu ndani ya watoto.
Nyumba salama, nyumba salama.
1
Msifu Mungu, Ee watoto wote, Yu pendo, Yu pendo;
Msifu, Msifu, Ee watoto wote Mungu ni upendo.
2
Tunampenda, Ee watoto wote, Yu pendo, Yu pendo,
Tunampenda, Ee watoto wote Mungu ni upendo.
3
Tumikeni, Ee watoto wote. Yu pendo, Yu pendo,
Tumikeni, Ee watoto wote Mungu ni upendo.
1
Mwokozi wangu alinipenda,
Maovu ayanitengi naye,
Alijitoa, kuniponya,
Sasa mimi wake.
Chorus
Mimi wake kabisa,
Naye Yesu wangu,
Si kwa wakati huu tu,
Bali na milele.
2
Dhambi nilijidhili sana,
Yesu akaja kunikomboa,
Akanitoa sumbukoni,
Sasa mimi wake.
3
Furaha nyingi moyoni mwangu,
Bwana Yesu kunifanya huru,
Kunitwaa kwa damu yake,
Sasa mimi wake.
1
Nani ayafanya maua, maua,
Nani ayafanya, Mungu juu.
2
Nani apambaye machweo, machweo,
Nani ayapamba, Ni Mungu.
3
Nani afanya theluji, theluji,
Nani aifanya, ni Mungu.
1
Nani afanya upindi,
Namjua, namjua
Mungu afanya upindi
Nampenda kwa hiyo.
2
Mungu atuma upindi
Ni bora mweupe,
Mungu atuma upindi,
Kwamba yu karibu.
1
Napenda sana kufika, skuli ya Sabato
Napenda sana kufika, skuli ya Sabato
2
Napenda sana kuimba, habari za Yesu,
Napenda sana kuimba, siku ya Sabato
3
Napenda sana kutoa, sadaka kwa Yesu,
Napenda sana kutoa, siku ya Sabato
4
Napenda sana kuomba, kwa Yesu, kwa Yesu,
Napenda sana kuomba, siku ya Sabato
5
Napenda sana kujua, maneno ya Yesu,
Napenda sana kujua, siku ya Sabato
6
Napenda sana kusema, Fungu la kariri,
Napenda sana kusema, siku ya Sabato
1
Roho wa Mungu wangu, Nakuhitaji!
Roho wa Mungu wangu, Nakuhitaji!
Unilinde na unijaze;
Roho wa Mungu wangu, Nakuhitaji!
1
Moyoni, moyoni; Ingia moyoni, Yesu.
Njoo leo, njoo kukaa, Ingia moyoni Bwana.
Moyoni, moyoni, Angaza moyoni Yesu,
Ng'aa leo siku zote, Angaza moyoni Bwana.
1
Mtazame Mwokozi,
Usoni Mwake mzuri,
Mambo ya dunia hugeuka,
Usowake tukiuona.
1
Niwe nao uzuri wa Mwokozi,
Nazo huruma Zake na usafi,
Roho Mtakatifu anibadilishe,
Aonekane Yesu ndani yangu.
1
Nataka niwe tayari, Bwana,
Nataka niwe tayari, Bwana,
Furaha za ulimwengu ni bure;
Nilinde hata uje!
1
Ulimwengu wataka kumwona Yesu;
Ulimwengu wataka kumwona Yesu.
Analeta furaha, shangilio kutosha,
Ulimwengu wataka kumwona Yesu.
1
Moyoni 'nijaze,
Na Roho wa Yesu;
Nataka kujitoa,
Moyoni 'nijaze.
1
Omba sana asubuhi,
Omba sana mchana,
Omba sana na jioni,
Bwana hutusikia.
2
Mungu hujibu maombi,
Asubuhi na mchana,
Hata hutungojea tena,
Wakati wa jioni.
3
Na tuimbe asubuhi.
Tena saa za mchana.
Hivi tutafurahi Naye.
Pumziko la jioni.
1
Yesu Mwokozi Mpendwa.
Hakuna mwingine!
Yesu Mwokozi Mpendwa,
Yesu Mwokozi Mpendwa,
Nakutazama wewe pekee,
Yesu Mwokozi Mpendwa,
Ninakutafuta;
Wewe u mali yangu.
Sasa na milele.
1
Pambazuka nuru,
Siku mpya yaja,
Basi amkeni na kuimba,
Ninyi nyote!
Pambazuka nuru,
Siku mpya yaja,
Yesu atakaporudi kama Mfalme!
1
Kwa heri, Mungu awalinde;
Kwa heri, na awaongoze;
Kwa heri, na kuwapa amani,
Bwana awabariki.