nyimbo-za-kristo-v4

103. Njoni Kwangu

edit

1
Yesu huita kwa upole mwingi, atwita wewe nami; Moyoni mwetu hungoja, hukesha, Hukungojea wewe.

Chorus
"Njoni kwangu, Mliochoka, njoni: Yesu huita kwa upole mwingi, Akwita, "uje kwangu"

2
Atuombeapo usikawie, Hutuombea sisi; Usidharau wema ma huruma, Huruma kwetu sisi.

3
Siku za maisha hupita hima, Hupita kwako, kwangu; Usiku waja, kifo kinakuja, Huja kwako na kwangu.

4
Fikiri juu ya upendo wake, Upendo kwako, kwangu; Dhambi zetu amekwisha samehe. Masamaha ni yetu.